2013-06-07 15:45:25

Papa aonya hatari za kuwa na miungu wadogowadogo kisirisiri


Baba Mtakatifu Fransisko, amewaonya Wakristu kutotunza miungu wadogowadogo wa kisirisri ambao huharibu maisha na mwenendo wao kwa Mungu mmoja. Onyo hilo alilitoa Alhamis,wakati wa Ibada ya Misa mapema Asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta. Alisema njia pekee iendayo kwa Mungu, ni kumpenda Mungu kama Yesu alivyofundisha.

Kama ilivyo desturi ya ikila siku kutoa tafakari ya masomo ya siku, ambamo somo la Injili lilieleza juu ya Mwandishi aliyemwendea Yesu na kuuliza ni ipi amri ya kwanza katika amri zote. Papa Fransisko alibainisha kwamba, pengine swali hili ni swali la hila la kumjaribu Yesu kama kwali analo jibu sahihi.

Maneno ya mwandishi huyo, yaliyonukuu Biblia, Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana peke yake! Na Yesu akamjibu na maneno , Wewe huko mbali na Ufalme wa Mungu. Papa Franssisko anasema kwamba, kwa maneno hayo, kwamba wewe si mbali na Ufalme wa Mungu, Yesu alitaka kumwambia mwandishi huyo, wewe unajua nadharia vizuri sana, lakini wewe bado uko mbali kutoka ufalme wa Mungu, maana kw amana kwamba, anahitaji kuongeza mwendo wa kubadilsiha amri hizi katika hali halisi za maisha , kwa sababu tunamkiri Mungu kupitia njia yetu ya maisha.

Haitoshi kusema lakini naamini katika Mungu, Mungu mmoja pekee. Hilo ni sawa, lakini ni jinsi gani unaweza kuishi hivyo katika safari ya maisha yako?Kwa sababu tunaweza kusema, 'Bwana ni Mungu mmoja tu, hakuna mwIngine,lakini hali halisi ya maisha yetu hazishuhudii uwepo wa Mungu pekee. Yanaonyesha uwepo wa miungu wengine katika makandokando yetu... Hii ni hatari, kwa kuwa miungu wengine hutuletea roho wa kidunia, roho wa tamaa, roho wa uchoyo, chuki, ubinafsi n.k.

Papa alikumbusha Yesu mwenyewe aliliweka wazi , hapana kwa Roho wa Kidunia katika sala yake ya wakati wa karamu ya mwisho, Baba utuopoe na roho wa ulimwengu, kwa sababu roho ya ulimwengu hutuongoza katika ibada za miungu wengine.

Papa Fransisko aliendelea: kuzungumzia ibada katika miungu wengine akisema sote tuna miungu wa kisirikisiri waliofichika lakini hujionyesha katika njia ya maisha ya tunayofuata. Na ili kuondokana na miungu hao wenye kutuweka mbali na ufalme wa Mungu ni kuwagundua miungu hawa wa kisirisiri waliofichika katika roho zetu.

Papa alieleza na kumrejea Rahel, mkewe Yakobo, aliye jifanya hana miungu wengine na kumbe, ana sanamu aliyochukua kutoka nyumba ya baba yake na kujificha katika matandiko yake. Papa alisema kwamba sisi pia "zimeficha miungu wetu wa sirisiri katika matandiko yetu ... inabidi kuwatafuta na kuwaangamiza kwa sababu njia pekee ya kumfuata Mungu ni njia ya upendo ambayo na msingi wa upendo huo, ni uaminifu.

Na uaminifu hutudai kuwafukuza miungu wote wadowadogo nje ya mioyo yetu, ambao huonekana katika tabia na mienendo yetu ya maisha. Mtume Yakobo anasema,.. Anayetaka kuwa mpenzi wa malimwengu, huwa adui wa Mungu.








All the contents on this site are copyrighted ©.