Italia yachanga kiasi cha Euro millioni 6 katika miradi ya kilimo
Serikali ya Italia imesema kwamba, itachangia kiasi cha Euro millioni 6 kwa ajili
ya kuendeleza mikakati ya maboresho ya sekta ya kilimo inayotekelezwa na Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO. Italia inagharimia miradi ya kilimo ipatayo
50 kwa kiasi cha dolla za Kimarekani millioni 127.2.
Italia ni kati ya nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika mikakati ya maboresho
ya sekta ya kilimo duniani. Mkazo mkubwa kwa sasa unaelekezwa katika harakati za kuhakikisha
kwamba, kuna uhakika na usalama wa chakula duniani, jambo ambalo linavaliwa njuga
na Italia kwa kushirikiana na FAO. Asilimia 40 ya fedha zote zinazotolewa na Italia
zinagharimia miradi ya kilimo Kusini mwa Jangwa la Sahara.