Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha watumiaji wa mitandao ya kijamii kwamba, ulaji
wa kupindukia umewatumbukiza watu wengi katika mazoea ya uharibifu wa chakula. Lakini,
ikumbukwe kwamba, chakula kinachotupwa ni sawa na kumwibia maskini na mwenye njaa!
Katika
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa Mwaka 2013, Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa
bwana Ban Ki-Moon ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuweka mikakati thabiti itakayosaidia
kudhibiti uharibifu wa chakula kama sehemu ya mbinu mkakati wa kupambana na baa la
njaa duniani.
FAO inabainisha kwamba, tani billioni 1.3 za chakula hutupwa
kila mwaka, wakati kuna mamillioni ya watu wanateseka na kufa kwa baa la njaa na utapimlo.