Ratiba ya Papa Francisko wakati wa Likizo ya Kiangazi yatolewa rasmi!
Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuanza likizo ya kipindi cha kiangazi kwa mwaka
2013 kwa kubaki mjini Vatican kwenye "Domus Sanctae Marthae. Kwa kipindi chote cha
mwezi Julai, Katekesi za Baba Mtakatifu kwa siku za jumatano zimefutwa. Ibada ya Misa
binafsi na wafanyakazi wa Vatican zinatarajiwa kuhitimishwa hapo tarehe 7 Julai 2013
na kuanza tena Mwezi Septemba, 2013. Hayo yameelezwa na Padre Federico Lombardi msemaji
mkuu wa Vatican.
Kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 29 Julai, Baba Mtakatifu Francisko
atashiriki katika Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013, inayoongozwa
na kauli mbiu "Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi" nchini Brazil.
Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa tarehe 14 Julai 2013 kusali pamoja na
waamini Sala ya Malaika wa Bwana, akiwa mjini Vatican.