Papa Fransisko alaani ukani Mungu kwamba ni hatari kwa jumuiya ya Kikristu.
Papa Fransisko Jumatatu akiongoza Ibada ya Misa ya Asubuhi, katika Kanisa dogo la
Mtakatifu Marta,homilia yake ililenga zaidi katika mambo matatu, dhambi, ukani Mungu
na utakatifu. Papa alisema, ukani Mungu, hufanya madhara makubwa kwa Kanisa, kwa
sababu mtu anayemkana Mungu, hujitukuza mwenyewe, kinyume na Watakatifu ambao hutenda
mengi kwa ajili ya manufaa ya wengi na kanisa. Hivyo Watakatifu ni mwanga wa maisha
adilifu ya Kanisa.
Papa alieleza hilo, kwa kurejea somo la Injili ambamo
alitaja kile kinachotakiwa kufanywa, kwa ajili ya kuwa wamiliki wa shamba la Bwana
la mizabibu. Alitaja makundiya matatu ya watu wanaoishi katika shamba la Bwana kuna
wenye dhambi, wakani Mungu, na watumishi wa Mungu. Papa alisema, hakuna haja
ya kuzungumzia sana dhambi, kwa sababu sisi wote ni wadhambi. Na hili tunalitambua
toka ndani ya mioyo yetu, na kama mtu hana hisia hizo kwamba ni mwenye dhambi, ajione
kuwa amepungukiwa na atafute msaada wa daktari wa kiroho. Aliendelea kuuchambua mfano
huo wa shamba la mizabibu, akimrejea mtu mwingine, anayetaka kumiliki shamba hilo
la mizabibu lakini kwa kupoteza uhusiano wake na Bwana wa shamba, Mwalimu ambaye,
ametuita kwa upendo, mwenye kutulinda na kutupatia uhuru kamili .
Papa alitahadharisha
hatari ya uhuru huo, unapokuwa katika mwelekeo wa kutaka kujitegemea, kujitenga
mbali na Mungu, na moyo wa kujiona umejikamilisha katika yote na hivyo kuona hakuna
haja ya Mungu kungilia kati maisha.. Moyo wenye kuwa na mwelekeo huo , hujenga ufisadi.
Na kwamba mafisadi hawa , walianza kuwa wadhambi kama sisi, Lna kuendeleea hadi kuongeza
hatua nyingine zaidi ya inayo wathibitisha katika dhambi yao, kuona hawana haja ya
Mungu, licha kwamba, kanuni asili ya maumbile ya binadamu katika uhusiano wake na
Mungu, haufutiki. Na kwa kuwa hawawezi kukanusha hili, wakani Mungu, hujitegenezea
miungu wa bandia, hivyo kuwa mafisadi wa imani.
Papa amewaasa kwamba, wakani
Mungu hujifikiria wenyewe tu , kuwa ndiyo kundi zuri. Lakini katika ukweli wake, hujilinganisha
wa maisha ya jamii ya Kikristo, ni watu walio jinasua wao wenyewe wamejinasua na
kujiweka nje. Papa alieleza na kutolea mfano wa Yuda aliye msaliti Yesu, ambaye kwanza
alitenda dhambi ya tamaa, na kupotelea katika ukani Mungu. Papa anaonya barabara
hii ya uhuru ni barabara ya hatari, ambamo wakani Mungu huwa wasahaulifu sana, husahau
upendo wa Bwana uliowapa kuwa wamiliki wa shamba la Bwana , na kuharibu uhusiano wao
na Bwana, na kujitenga na mahusiano na upendo huu, na kuwa na tabia ya kujiabudu wenyewe.
Ukana Mungu huu ni hatari kubwa katika jamii ya Kikristo! Papa amemwomba Bwana awaokoe
Wakristu wote wakati wanapotembea katika barabara hii ya imani ili wasitelezee chini
katika barabara ya ukani Mungu.
Papa alikamilisha hotuba yake kwa kurejea
maadhimisho ya miaka hamsini ya kifo cha Papa Yohane XXIII, "mfano wa utakatifu."
Katika Injili ya leo, aliongeza, Watakatifu ni wale waliokwenda kukusanya kodi katika
shamba la Bwana, wakijua Bwana wao anachokitarajia kutoka kwao, na wakafanya kila
jitihadi ya kutimiza wajibu wao. Watakatifu ni wale wanao Mtii Bwana, watu wa ibada
kwa Bwana, ni wale ambao bado hawajapoteza kumbukumbu ya upendo wa Bwana, aliyewaweka
katika shamba lake la mizabibu, hawa ndiyo watakatifu katika Kanisa. Kama ilivyo
ukani Mungu huleta madhara mengi kwa Kanisa,ndivyo ilivyo kwa Watakatifu hufanya mambo
mengi mazuri. Mtume Yohana anasema "Ukani Mungu ni adui wa Kristo, ingawa wao hutoka
miongoni mwetu na kuishi kati yetu, lakini wao wanakuwa tena si wa kwetu." Katika
Ibada hiyo , Papa aliomba kwa Bwana, neema ya kuelewa kwamba sisi ni wenye dhambi,
wadhambi wa kweli katika asili yake.. Lakini si wakani Mungu.Pia aliomba Neema ya
kutembea katika njia ya utakatifu. Na iwe hivyo. "
Katika Ibada hii, Papa aliongoza
Ibada akisaidiana na Kardinali Angelo Amato, Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Maisha Matakatifu
na ilihudhuriwa na kundi la Maaskofu, mapadre na kikundi cha maofisa kutoka jengo
la Kipapa.