Jumapili 2 June, mamilioni ya wakatoliki duniani kote walijumuika katika makanisa
wakitolea muda wao katika saa ya Kuabudu Ekaristi Takatifu, kama alivyoomba Papa Fransisko,
dunia ya waamini wote wka pamoja majira ya saa kumi na moja na nusu za jioni, wawe
mbele ya Kristu aliye hai ndani ya Ekaristi Takatifu. Papa Fransisko , aliliongoza
tukio la hili, bila ya kutazamiwa, katika Kanisa Kuu Mtakatifu Petro la Vatican.
Watu waliweza pia kufuatilia tukio hili, katika njia za mawasiliano jamii, televisheni,
redio na mtandao wa internet. Baba Mtakatifu aliomba wakati huu wa Kuabudu Ekaristi,
maombi yatolewe ili kwamba, Kanisa liweze kuenea duniani kote , na katika mjumuiya
wa waamini kwa wakati mmoja , saa ya ibada kwa Ekaristi Takatifu, iwe ishara ya umoja
wa Wakristu. Papa alisali ili kwamba Bwana, awezeshe Kanisa kuwa tiifu zaidi katika
kusikia Neno la Bwana, na ili uziri wake uweze kung'ara mbele dunia kwa watu wote
kuona manufaa yake, bila ya kupakazwa na matope ya dhambi na kashfa, lakini likiwa
takatifu na bila lawama zisizokuwa na misingi. Pia Ili kwamba, kupitia tangazo
lake aminifu,juu ya Neno linalo okoa wengi, liendelee kutoa mwangi wa huruma ya Mungu
na kuongeza upendo katika kupata maana kamili ya maumivu na mateso, kwamba ni furaha
na utulivu. Na ili kwamba, kwa wale wote ambao hata leo hii, wapo katika pande
mbalimbali za dunia, ambao bado wanakabiliwa na mateso ya hali , au kuathiriwa na
vita, biashara ya binadamu, soko la madawa ya kulevya, na sulubu ya kazi ngumu za
kitumwa, waweze kuuona mwanga wa kuokoka katika mateso hayo. Papa pia alitolea sala
kwa ajili ya watoto na wanawake wanaokabiliwa na maisha magumu na hatarishi kutokana
na kila aina ya vurugu na madhulumu. Pia aliomba ili kwamba, ukelele wa kimyakimya
unaotafuta msaada, uweze kusikika na kusikilizwa na Kanisa hai, linalo mkazia sana
macho Kristu Msulubiwa, lisiweze kuwasahau ndugu hawa wake kwa waume, walio sahaulika
na kuachwa katika huruma ya vurugu. Pia, kwa wale wanaojikuta katika hali halisi
ngumu za kiuchumi, hasa katika kupambana na ukosefu wa ajira, wazee, wahamiaji, wasio
na makazi, wafungwa, na wale wote wanaobaguliwa na kunyanyasika katika jamii kutokana
na hali zao duni. Ili kwamba sala ya Kanisa na juhudi zake za kuwafariji na kuwapa
msaada katika tumaini, zipate nguvu na ujasiri katika kutetea hadhi ya kila binadamu.
Ibada
ya kuabudu Ekaristi Takatifu , iliongozwa na somo la Injili ya Yohane sura ya sita,
ambamo Yesu anazungumzia Ekaristi. Ibada hiyo pia ilipambwa kwa nyimbo za kijadi juu
ya Ekaristi. Na pia kulitolewa maombi ya Mapapa sita tangu wa Papa Pius XII hadi
Papa Benedict XVI, wakati huo wa kuabudu, na pia kwa ajili ya mahitaji mengine ya
wanadamu wote.
sherehe alihitimisha kwa Wimbo wa "Tantum Ergo" na Baraka Takatifu
za Ekaristi iliyobarikiwa na Papa Francis.