Jumapili, Baba Mtakatifu Fransisko, akiuhutubia umati wa waamini mahujaji na wageni
zaidi ya laki moja, waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,
nyakati za Sala ya Malaika wa Bwana, aliwaaambia, Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Kristu
, inatuita katika wogofu wa matumaini, kuweza kugawa kidogo tulicho nacho na kamwe
tusibaki tumejifungia wenyewe ndani kwa woga wa kuishiwa..
Papa alitoa hotuba
yake akiirejea Siku Kuu ya Alhamis, ambayo ilikuwa ni Maadhmisho ya Mwili na Damu
ya Kristu ( Corpus Christi), ambayo nchini Italia na pia katika mataifa mengine
mengi, iliadhimishwa rasmi siku ya Jumapili. Papa Katika hotuba yake alirejea
somo ya Injili, juu ya muujiza wa mikate (Luka 9:11-17), akilenga zaidi katika hali
ilivyokuwa siku hiyo katika pwani ya Ziwa Galilaya, ambako jioni inajongea na watu
wengi bado wamekusanyika kwa Yesu kw amuda wa saa nyingi na hivyo wana njaa. Na wanafuzi
wa Yesu wajadiliana juu ya tatizo la watu hao watakula nini, na hivyo kumuomba Yesu,
atawanye watu ,ili kila mmoja atafute mbinu zake za kujipatia chakula. Lakini Yesu
anawajibu, Wapeni ninyi chakula (mstari 13). wanafunzi ni kwa haraka nao wakajibu
tuna mikate mitano na samaki wawili, wa kuwatosha wao.
Papa Fransisko alisema,
Yesu alijua vizuri sana nini cha kufanya, lakini alitaka kuwahusisha wanafunzi wake,
alitaka kuwafundisha, kwamba Mtazamo wao wanafunzi ni wa kibinadamu, unaotafuta ufumbuzi
wa tatizo katika hali halisi na jawabu la kibinadamu lisilotaka kuzua matatizo mengine.
Waache watu waende zao, ili kila mmoja ajipangie atakula nini. Na pia wanafunzi walimhurumia
Yesu wakitaka apate muda wa kupumzika., kwa kuwa alikuwa tayari kafanya mengi kwa
ajili yao , kuwahubiri na kuwaponya wagonjwa. Na sasa basi waache waende zao.
Mtazamo
wa Yesu, kwa wanafunzi wake, unakuwa tofauti kabisa. Yesu anaonyesha kuwa na muungano
na Baba yake wa huruma kwa watu. Yesu mwenye huruma, anayajua matatizo yao, mapungufu
yao, na mahitaji ya watu, na ndivyo ilivyo hata kwetu sisi sote. Yesu aliiona
hiyo mikate mitano , kuwa tayari ni riziki , kwamba kutoka vitu hivi vichache, Mungu
anaweza kuzalisha kile ambacho ni muhimu kwa kila mtu. Yesu anaiweka imani yake kamili
kwa Baba wa Mbinguni kwa utambuzi thabiti kwamba kwa Yeye kila jambo linawezekana
. Na hivyo anawaagiza wanafunzi wake , kuwaketisha watu katika makundi ya watu hamisini
hamsini. Papa anafafanua , watu kuketishwa katika makundi makundi ya watu hamisni
hamsini si tu ilifanyika bila lengo lakini ilimaanisha makundi makundi hayo si tena
makundi ya watu ya kawaida lakini inakuwa ni jumuiya inayolishwa kwa Mkate wa Mungu.
Yesu aliitwaa mikate na samaki wawili akiinua macho yake mbinguni, na kubariki.
Papa anasema rejea ya tukio hili kwa Ekaristi ni dhahiri , kisha akaumenga mkate
na kuwapa wanafunzi wake na wanafunzi wake waligawa mikate na samaki kwa watu wote
bila kwisha. Walikula wote na kusaza. Hii inakuwa ni ishara ya Yesu , kuwa ndiye Mkate
wa Mungu kwa Binadamu.
Wanafunzi wake waliona, lakini hawakuelewa ujumbe wake
vizuri. Walimezwa na shauku za mshangao, jinsi ilivyowezekana kuulisha umati huo wa
watu kwa mikate mitano na samaki wawili. Kwa mara ingine tena, wanafunzi walijawa
na fikira za kibindamu na si zile za kimungu, kwamba , ujumbe mzima ni huduma, upendo
na imani. Kwa muujiza huu, tunaapaswa kujifunza kwamba, Siku Kuu ya Mwili na Damu
ya Kristu , hutualika sisi sote kuongekea imani katika matumaini , kushirikishana
na kugwana kidogo kilichopo au kile tunachoweza kupata na wengine na kamwe tusijifungie
kwa woga wa kuishiwa. Papa alimalizia hotuba yake kwa kuomba msaada wa Mama Maria,
atusaidie kuwa imara katika uongofu huu, na kweli kuwa wafuasi wa Yesu, tunaye mwabudu
katika Ekaristi. Amina.