imepita miaka hamsini tangu alipofariki Papa Yohane XIII
Jumatatu hii, June 3, imetimia miaka hamsini kamili, tangu Mwenye Yohane XXIII, alipofariki
duniani. Mwenye Heri Yohane XIII, kabla ya kuwa Papa aliitwa Angelo Giuseppe RONCALLI
alifariki dunia Juni 3, 1963, ikiwa miezi miwili baada ya kukamilisha waraka wake
maalum wa kichungaji juu ya Amani Duniani (Pacem in Terris). Papa Yohana XIII,
alichaguliwa kuwa Khalifa wa Kiti cha Petro tarehe 28 Oktoba 1958 katika umri wa
miaka 77. Inaelezwa wakati wa kuchaguliwa kwake, wengi walimwona kama ni Papa mlezi...
Lakini alishangaza wengi kwamba katika kipindi cha utawala wake wa miaka minne na
nusu kama Papa na Askofu wa Roma, alizindua mengi kwa Kanisa Katoliki, moja wapo ikiwa
ni kuitisha kwa Mkutano Mkuu wa Pili wa Vatican.