2013-05-31 08:46:19

Unganeni na Baba Mtakatifu Francisko katika Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu! Mshirikisheni Yesu: hofu na wasi wasi zilizomo mioyoni mwenu!


Askofu mkuu Paul Ruzoka, Mwenyekiti wa Tume ya haki na amani, Baraza la Maaskofu Katoliki anawaalika waamini kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Ekaristi Takatifu sanjari na kufanya Ibada ya Kuabudu, kama kielelezo cha mshikamano wa imani na Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili ijayo kuanzia saa Saa 12:00 hadi Saa 1:00 kwa saa za Afrika Mashariki. RealAudioMP3

Kama sehemu ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Baba Mtakatifu Francisko ataungana na Wakatoliki sehemu mbali mbali za dunia kusali na kuabudu mbele ya Ekaristi Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Askofu mkuu Paul Ruzoka anasema kwamba, hii itakuwa ni nafasi kwa waamini kuweza kusali kwa ajili ya kuombea amani, upendo na mshikamano. Waamini wasali ili Mwenyezi Mungu aweze kuwaepushia hatari zote, mashaka na wasi wasi kwa kila mwamini mmoja mmoja na taifa katika ujumla wao.

Anawaalika waamini kufuata utaratibu uliopangwa kwenye Majimbo husika, ili kuonesha mshikamano na umoja katika Bwana mmoja na Imani moja, kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho ya Ibada hii ya Kuabudu Ekaristi Takatifu, Jumapili ijayo, tarehe 2 Juni 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.