Taarifa imetolewa kwamba, Papa Fransisko, atatembelea Assisi Oktoba 4 , 2013, ambayo
NI Siku Kuu ya Mtakatifu Francis, mlezi wa Italia. Askofu Mkuu wa Assisi-Nocera
Umbra-Gualdo Tadino, Msgr. Domenico Sorrentino, ametangaza hilo, na kueleza kwamba,
katika maadhmisho hayo, kengele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Fransisko, litapigwa kwa
muda mrefu, kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa majaliwa ya Mungu na pia kama ishara
ya furaha ya kutembelewa na Papa Fransisko. Askofu Mkuu Sorrentino anasema, ziara
hii ya Papa Fransisko kutembelea eneo lao, wanaipokea kuwa ni kitendo cha heshima
na thamani sana, kitakacho ongeza nguvu ya kiroho kwa wakazi wa eneo hili. Itakuwa
ni siku nzuri, ya tumaini na neema kubwa, kama ambavyo ni tayari anajionyesha kwa
Kanisa zima, kwa njia ya ushuhuda wake wa maisha na maneno yake. Hii itakuwa zaidi
kuwaimarisha Wafransiskano tu lakini pia kukutana watu maskini wa mji wa Assisi,
ushahidi wazi Mtakatifu Francsisko wa Assisi.