2013-05-24 15:26:13

Kuweni Chumvi ya Dunia na msipoteze ladha yake


Ili kwamba Wakristo waweza kueneza chumvi ya imani, matumaini na upendo kiroho. Ni Ujumbe wa Papa Fransisko katika Ibada ya Misa ya Alhamis asubuhi katika Kanisa ndogo la Mtakatifu Marta la ndani ya Vatican. Papa alionya Waamini dhidi ya hatari ya kupoteza ladha katika imani na kuwa sawa na bango la Makumbusho ya Ukristo. Kati ya waliohudhuria Ibada hii ni pamoja na Kardinali Angelo Sodano na Kardinali Leonardi Sandri , na pia kikundi cha Mpadre na walei kutoka Mkanisa ya Mashariki.
Katika hotuba yake, Papa Francis ililenga katika maisha halisi ya Mkristu akisema kila Mkristu ameitwa kutatolea sadaka maisha yake mwenyewe na kwa ajili ya wengine. Na kwamba chumvi ya kiroho inayotolewa na Bwana ni chumvi ya imani, matumaini na mapendo. Lakini ni lazima kuwa waangalifu kwamba,ili kwamba chumvi hii , tuliyopewa katika kuwa na uhakika kwamba Yesu alikufa na kufufuka ili kutuokoa, haipotezi ladha yake, wala kupoteza nguvu yake. Hii chumvi, si ya kuiihifadhi kama akiba kwa ajili yetu wenyewe, kwa kuwa chumvi kama ilivyo inayohifadhiwa katika chupa, hubaki kama ilivyo , bila kukipa ladha chakula hata kiicho karibu na hiiyo bila kutumika inakuwa haifai kitu.
Papa alieleza juu ya mantiki ya chumvi katika kukifanya chakula kuwa kitamu zaidi na njisi isivyo tunzwa inavyopoteza nguvu yake akianisha na uhalisi w aMkristu katika hili , kwamba kila mmoja kwa njia ya ubatizo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu hufanywa kwua ladha ya maisha matakatifu katika jamii kama chumvi ilivyo katika chakula. "
Uhalisi huu wa Mkristo ni mzuri, kwa sababu, huejnga mshikamano na wengine. Na hivyo kila Mkristu katika uhalisi wake , anakwua ni zawadi ya wengine kutoka kwa Bwana katika kuyafurahia maisha.

"Papa aliendelea kubaini kwamba, chumvi ambayo tunaipokea kutoka kwa Bwana ni chumvi inayotakiwa kutolewa na si ya kuwekwa, lakini kutolewa. Na kwamba ni Kwanza: kutoa chumvi "katika huduma ya chakula huduma, kwa wengine, kwa mana ya kutumikia watu. Pili ni kuendelea kuwa bora bila kuchuchuka katika kumwelekea Muumba wa chumvi, ili kuweka ladha yake , si tu katika njia ya mahubiri, lakini pia mahitaji mengine ya sala na kuabudu.
Kwa njia hii chumvi hubaki na ladha yake . Na ibada kwa Bwana humfanya muumini kuzama zaidi ufahamu wake mwenyewe kwa Bwana,na kwenda kuitangaza Injili na kutoa ujumbe wake. Kama hatuwezi kufanya hilo, basi onjo la furaha ya kuwa Mkristu tulilopewa wakati wa Ubatizo hubaki limefungiwa ndani mwetu kama ilivyo chumvi iliyofunguìiwa katiak chupa, na hivyo muumini hubaki kuwa kama bango la makumbusho la Wakristo.
Papa anasema , tunaweza kuonyesha ladha ya chumvi hii na jinsi ilivyo nzuri , chumvi tuliyoipokea wakati wa ubatizo , au wakati wa kupokea Kipaimara, au katika kusikiliza katekesi - lakini tazama, kama hatatumika kama onjo la kuhamasisha wengine kuja kwa Kristu, inabaki kuwa sawa na kipande cha bango la makumbusho la Mkristu, kuwa chumvi isiyotumika iliyofungiwa ndani ya chupa na haina ladha yoyote.








All the contents on this site are copyrighted ©.