2013-05-24 15:36:20

Kuwa Mchungaji maana yake ni kuamini katika neema na nguvu zinazo toka kwa Bwana.


Baba Mtakatifu Alhamis akihutubia Maaskofu Katoliki wa Italia, alizungumzia unyenyekevu na utiii wa Askofu kama Mchungaji kwamba, maana yake ni kuamini kila siku, katika neema na nguvu ambayo inatolewa kwao na Bwana, licha ya udhaifu wao. Ni kutambua kikamilifu jukumu lao la kutembea mbele ya kundi kwa uhuru na kukubali kubeba mizigo na kutafuta kila mbinu za kuzuia changamoto zinazozuia kazi za kitume kustawi, na bila kusita katika kuongoza, na kufanya sauti ya Kanisa kusikika na kumtambuliwa na watu wote ili waweze kuvutiwa imani, hata wale walio nje ya zizi.
Kwa hiyo, kuwa wachungaji ina maana pia kuwa tayari kutembea katikati na nyuma ya kundi: kuwa na uwezo wa kusikiliza maelezo kimya kimya juu ya mateso na kutafuta ufumbuzi wa matatizo hatua kwa hatua hadi hofu itoweke na kuhakikisha na kuhamasisha matumaini.
Na kwamba, kwa kushirikishana pamoja imani ya unyenyekevu,daima huimarika kiimani na kuweka kando, aina zote za kiburi, na kuwa wamoja katika kumwelekea Bwana aliye wakabidhi huduma ya kuwa Wachungaji.

Ni maelezo ya Papa katika hotuba yake ya siku ya Alhamsi kwa Maaskofu wa Italia, walikusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wao Mkuu wa 65. Papa Fransisko alijiungana na Maaskofu hao kutolea sala na kukiri imani , na alitoa tafakari fupi , baada ya Kardinali Angelo Bagnasco, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, kufungua Mkutano ikifuatiwa na Liturujia ya Neno. Katika hitimisho la Ibada hii ya masifu ya jioni, Papa Fransisko aliwaongoza Maaskofu, kukiri imani.
Tafakari ya Papa Fransisko juu ya liturujia ya Neno lililosomwa, ilitazamisha Maaskofu katika kuona umuhimu wa kuuanza mkutano wao ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro akisema si tu ni mahali panapotunza na kulinda kaburi la Mtakatifu Petro, lakini pia hudumisha kumbukumbu ya maisha ya ushuhuda wake wa imani, wa huduma yake ya kweli, na zawadi ya yeye aliyoyatolea maisha yake toa mwenyewe – hadi kuuawa - kwa ajili ya Injili na kwa ajili ya Kanisa.

Papa aliiyataja madhabahu hii ya wongofu kuwa sawa na ziwa la Tiberia, ambamo katika mwambao wake, wanasikiliza kwa mshangao mazungumzo ya ajabu kati Yesu na Petro , na maswali juu aliyoulizwa Mtume Petro ambayo kwa sasa yanakuwa ni maswali yanayotakiwa kusikika katika kila moyo wa muumini na mioyo ya Maaskofu.
Papa alieleza hayo akitazamisha katika swali la Yetu kwa Mtume Petro, “Simoni Mwana wa Yohane , Je Wanipenda mimi kuliko hawa Taz. Yn 21:15 . Swali lililorudiwa na Yesu kwa mara kadhaa.

Papa aliwaambia Maaskofu ni swali linapaswa kujibiwa na kila mmoja wao, na hakuna namna ya kuliepuka, na kwamba katika undani wake, bila kutoa jibu kwa haraka sana na bila kufikiri sana, ni swali linalo hamasisha moyo wa kumtazama Yesu kwa makini, na kujichunguza na kutoa jibu la ndani la kweli kama kweli tunampenda Yesu kuliko vyote.








All the contents on this site are copyrighted ©.