Mapema Alhamis hii, katika ukumbi wa Kitume wa Vatican, Papa alikutana na Rais wa
Jamhuri ya El Salvador Mheshimiwa Rais Carlos Mauricio Funes Cartagena. Na baadaye
Rais huyo alikutana na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu wa Jimbo, akifuatana na
Askofu Mkuu Dominique Mamberti, Katibu wa Mahusiano na Marekani. Wakati wa mazungumzo
yao yaliyofanyika kaitka hali ya kirafiki na maelewano , walitazama zaidi mahusiano
mazuri yaliyopo , kati ya Jimbo Takatifu na Jimbo la El Salvador. Na pia waliyatazama
maisha ya mtumishi wa Mungu, aliyewahi Askofu Mkuu wa San Salvador, AskofuMkuu Oscar
Arnulfo Romero y Galdà mez , na umuhimu wa shuhuda zake, kwa ajili ya taifa zima la
an Salvador. .
Na walipongeza mchango Kanisa unaofanikisha maridhiano na uimarishaji
wa amani, na pia kupitia maeneo ya huduma ya elimu, na miradi ya kutokomeza umaskini
na uhalifu wa kupangwa. Na pia walitazama baadhi ya masuala ya kimaadili kama vile
ulinzi wa maisha ya binadamu, ndoa na familia. Papa amthibitisha Kardinali
Vallini kuwa Vika Mkuu wa Jimbo la Roma. Aidha mapema Asubuhi hii, ilitolewa
barua ya Papa Fransisko iliyoandikwa kwa lugha ya Kilatini, inayo mthibitisha Kardinali
AUGUSTINO VALLINI, kuwa Vika wa Jimbo la Roma.