Ukuu wa madaraka hata ndani ya kanisa ni kuhudumia wengine.
Hata ndani ya kanisa, ukuu wa maradaka umo katika kuhudumia wengine, ni ujumbe wa
Papa kwa wote wanaotafuta kupanda ngazi katika madaraka na vyeo. Papa anasema,
hata ndani ya Kanisa, njia pekee ya kusonga mbele ni kutumikia na si kutumikiwa kwa
kuwa, kwa Mkristo, maendeleo katika mamlaka maana yake ni kuwa myenyekevu zaidi katika
kuhudumia , kama Yesu alivyokuwa. Papa pia alisisitiza kuwa, nguvu ya kweli ni huduma
na si bidii za kutafuta vyeo katika mamlaka . Papa Fransisko alieleza katika
mahubiri yake ya wakati wa Ibada ya Misa, asubuhi Jumanne , katika Kanisa ndogo la
Mtakatifu Marta ndani ya Vatican. Kati ya walioshiriki katika Ibada hii ni pamoja
na Mkurugenzi wa mipango wa Radio Vatican, Padre Andrzej Koprowski aliyeandamana
na wafanyakazi wa Redio Vatican na ofisi za utawala za Vatican na mahujaji na watalii
kadhaa. Pia walikuwepo Maria Voce na Giarncarlo Falletti ambao ni Rais na Makamuw
a Rais wa Kikundi cha Fokolare. Katika homilia yake, Papa alisema, kwa Mkristu
maendeleo ya kweli hupatikana katika unyenyekevu binafsi, kama Yesu alivyokuwa. uwezo
na nguvu ya kweli katika utendaji ni katika huduma na kwamba hakuna nafasi ya nguvu
ya mapambano ndani ya Kanisa.
Papa aliendelea kuyatafakari masomo ya siku
akisema, katika somo la Injili ,Yesu anazungumza juu ya mateso yake mwenyewe. Hata
hivyo wanafunzi wake, hawakuelewa na walianza kubishana kuhusu nani aliye mkuu kati
yao. Papa akizungumza juu ya sehemu hii yenye machungu, alibainisha kuwa utafutaji
wa kuwa mkuu katika madaraka hata ndani ya kanisa, si jambo jipya, kwa kuwa lilikuwepo
hata tangu wakati wa Yesu, kama ilivyosikika katika somo la Injili. Na Yesu anatoa
jibu katika mabishano hayo akisema, anayetaka kuwa mkubwa kuliko wote na awe mtumishi
wa wote. Kwa jibu hili, Yesu anatupa fundisho kwamba,uwezo na nguvu ya madaraka ndani
ya kanisa ni huduma. Uwezo wa mamlaka katika utumishi, unajionyesha katika uhalisi
wake kwamba ni huduma, kama yeye mwenyewwe alivyosema, sikuja kutumikiwa ila kutumikia
na huduma yake ilikuwa huduma ya Msalaba , ambako alijinyenyekeza hata mauti, naa,
mauti ya msalaba kwa ajili yetu, ili kutukomboa sisi. Na hivyo kwa sisi wafuasi wake
, hakuna njia nyingine katika Kanisa ya kusonga mbele ila kupitia huduma. . Kwa
Mkristo maendeleo yake hupatikana katika unyenyekevu wa huduma yake. Kama hatuwezi
kujifunza sheria hii ya Kristo, sisi kamwe, hatuwezi kuuelewa ukweli wa ujumbe wa
uwezo wa Yesu.
Papa alisema kuwa maendeleo "ina maana ya kuwa myenyekevu,
kwa maana ya daima kuwa tayari kuhudumia wengine. Katika Kanisa, aliongeza, mkubwa
ni yule anayekuwa mtumishi wa wengi, ni mtu aliye tayari kuhudumia wengine. Hii
ni sheria. Hata hivyo, alibainisha Papa Fransisko kwamba, tangu mwanzo wa kanisa
mpaka sasa kumekuwa na mapambano ya kutafuta ukubwa ndani ya kanisa na katika huduma
za kijamii , wengi wakidhani kuw amkubwa ni kutumikiwa, kama inavyojionyesha katika
namna za mazungumzo kwa wanao utafuta ukubwa.
Papa alizigeukia pia hali
za kawaida za kijamii akisema, mtu anapopewa cheo kikubwa kinachotupiwa macho na
wengi , wengi humwonea kijicho wakisema ah, mwanamke huyu au baba huyu ameula kwa
kuwa sasa ni rais wa chama. Neno hili kupandishwa cheo ni nzuri na tunalitumia pia
katika kanisa. Lakini maana halisi ya kupanda cheo ni kubebeshwa msalaba. Anayekubali
kupandishwa cheo, anapaswa kujua kwamba , sasa anatakiwa kuwa mnyenyekevu zaidi kuliko
alivyokuwa hata awali. Ni kukubali kuwa mnyenyekevu zaidi kwa ajili ya kuhudumia
wengi zaidi. Huo ndio ukweli wa maana ya kupanda cheo . Papa kisha alikumbuka
kwamba Mtakatifu Inyasi wa Loyola ambaye, katika mazoezi yake ya kiroho, aliomba kwa
Bwana Msulubiwa, neema ya unyeunyekevu. Na hii, alisisitiza ndiyo nguvu ya kweli ya
huduma ya Kanisa. Hii ndiyo njia ya kweli ya Yesu,. Kama Yeye ulivyo hudumia, pia
ni lazima kwa Mkristu kumfuata katika njia hii ya huduma. Hiyo ndiyo nguvu ya
uweza wote wa huduma kwa Kanisa.
Papa alieleza na kutolea sala ili kwamba,
Bwana Mfufuka awajalie wafuasi wake wote neema kuelewa kwamba: uweza na nguvu halisi
katika kanisa ni huduma. Na pia kuelewa kwamba, Sheria kuu aliyotufundisha katika
mfano wa maisha yake kwa ajili ya maendeleo ya Mkristo, ni unyenyekevu.