Baba Mtakatifu Fransisko, katika katekesi yake kwa mahujaji na wageni, Jumatano hii,
ameendelea kuitaza imani ya muumini kwa makini akisema," ndugu zangu wapendwa: katika
katekesi yetu juu ya Imani, kwa sasa tunaingia katika kipengere cha Roho Mtakatifu
kwa Kanisa moja, takatifu, katoliki na la kitume. Roho Mtakatifu anaye huisha na kuliongoza
Kanisa na kila muumini aliye ndani ya kanisa kutekeleza agizo la Kristu la kuwafanya
watu wote kuwa wanafunzi wake".. Papa aliendelea kueleza kuwa, Roho Mtakatifu
huifungua akili na mioyo katika kuuona uzuri na ukweli wa Injili. Roho mwenye kuvishinda
vishawishi vya kuwa na ubinafsi na mgawanyiko, mwenye kujenga umoja, mshikamano,
maridhiano na upendo. Roho mwenye kutia nguvu zinazohitajika katika kuwa na ushupavu
wa kumshuhudia Kristu Mfufuka. Roho wa missioni na uinjilishaji. Na kwamba, moto
wa Roho Mtakatifu, ulimiminwa juu ya mitume siku ya Pentekoste, kama zawadi na jibu
la kuomba kwa biidii. Roho Mtakatifu, jibu kwa Roho ya kina katika maombi, inakuwa
daima ni nafsi ya uinjilishaji mpya na roho wa maisha yetu kama wakristo. Papa
alieleza na kusali ili kwamba kila siku waamini waruhusu Roho Mtakatifu kufanya
kazi ndani mwao, akiifanya upya imani, na kuifungua mioyo na kuvuviwa na zawadi
zake na kujitahidi kuwa ishara ya umoja na ushirika na Mungu katikati ya familia
ya binadamu. Baada ya homilia yake Papa aliwaalika wote kusali pamoja naye, kwa
nia ya kuwaombea waathirika wa maafa yaliyotokea kibunga kilichotokea Oklahoma.Alisali
ili kwamba, Bwana mwenyewe na amfariji kila mmoja wao, na hasa wazazi walio poteza
watoto katika tukio hili la kutisha. Pia aliwakaribisha mahujaji wanaozungumza
Kiingereza-kutoka Uingereza, Ireland, India, Canada na Marekani. Na alitoa salaam
zake za kipekee kwa mahujaji kutoka Jimbo Kuu la Hartford na Chama Cha Wanafunzi kutoka
Chuo Kikuu cha Kikatoliki ya Amerika. Na mwisho aliwapa baraka zake za Kitume ,
kwa wao wenyewe na kwa familia zao, na zawadi pekee ya hekima na ya amani ya Roho
Mtakatifu akisema, Mungu awabariki wote!