2013-05-22 09:32:08

Papa alikuwa anamwombea mgonjwa!


Baba Mtakatifu Francisko hana mpango wa kuwatoa wagonjwa mapepo, kama walivyodai baadhi ya waandishi wa habari kwa siku za hivi karibuni, walipomwona Baba Mtakatifu akimwekea mgonjwa mikono juu ya kichwa chake alama ya kumwombea. Ni ufafanuzi unaotolewa na Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican.

Baba Mtakatifu anapokutana na wagonjwa anawaombea na kusali pamoja nao na kwamba, kitendo cha Baba Mtakatifu Francisko kumwekea mgonjwa mikono kichwani haikuwa ni alama ya kutaka kumtoa mapepo au kumfanyia miuujiza.







All the contents on this site are copyrighted ©.