2013-05-21 15:10:16

Wabudha na Wakristu wakutana katika meza ya majadiliano Roma.



Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo kati ya dini , kwa kushirikiana na Ofisi ya Kiekumeni na Tume ya Mazungumzano kati ya dini ya Baraza la Maaskofu la Italia, waliendesha Mkutano wa Nne wa Pamoja, Wabudha na Wakristu, katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana cha Mjni Roma, chini ya kaulimbiu "Amani ya Ndani, Amani kati ya watu."
Washiriki wa mkutano huu, wanashuhudia kwamba, mkutano ulifanyika katika hali ya majadiliano ya kirafiki , hata nje ya majadiliano rasmi na hivyo kuwezesha kushirikishana ufahamu na maoni ya kina kwa kila mmoja kuuelewa utamaduni wa mwingine , kujua vyema faida za mshikamano na umoja na yale yanayo watofautisha, na kuwa na ufahamu wa pande zote katika wajibu wao wa kurejesha amani na kuidumisha.

Washiriki wa Mkutano huu walitoka Italia, Japan, Vietnam Jamhuri ya China (Taiwan),Korea, Thailand, Myanmar, Sri Lanka na India, mchanganyiko ulioonyesha kwamba dunia inabadilika haraka sana. Na katika mazingira kwamba, wafuasi wa mila za dini mbalimbali, wanaweza kuchanganyika katika hali ya urafiki na mshikamano, ni jambo la kutia moyo kwamba haki na amani vinaweza kupatikana duniani.

Tamko kutoka mkutano huo linasema bayana kwamba, Kwa Wakristo, dhambi ni katika hali zake zote za ubinafsi na ukatili, uchoyo na tamaa ya kufanya maasi yanayotafuta kutawala kwa mabavu, kutovumilia wengine,kujenga chuki na miundo yote ya madhulumu kwa binadamu wengine. Hayo yote hurarua muungano uliopo kati mtu na Mungu na sisi kwa sisi. Hivyo marejesho ya amani, linakuwa ni sharti msingi katika kujiweka huru dhidi ya dhambi na tamaa zake.
Yesu Kristo alikuja kwa ajili ya kurejesha uhusiano kati ya Mungu na Binadamu uliovurugwa binadamu anapo tenda dhambi.Kwa kumwamini na kuzifuata sheria za Kristu, binadamu hukumbolewa na kuwekwa huru dhidi ya dhambi.
Nae Buddha Sakyamuni akizungumza kwa niaba ya upande wa Mabudha alisema kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao, mzizi wa maovu yote ni ujinga na maoni ya uongo yaliyosimikwa katika misingi ya uchoyo, chuki na madhulumu . Nakwmba kinyume chake ni kungundua njia nne za ukweli katika kujiweka mbali na mateso na kuwa mtu huru. Alitaja njia hizo ni uadilifu na usafi wa akili , na pia mazoezi ya kimwili ikiambatana na mapumziko na utulivu wa kutafakari na kufanya kazi kwa ajili ya ukombozi wa Viumbe. Ni kuepukana na mateso endelevu kwa kutembea katika njia ya inayoongozwa na hekima. Na kwamba, kwa kweli halisi, ubudha ni kuwa na huruma kwa wengine , huruma inayotokana na mwamko wa utambuzi mkubwa wa umoja wa viumbe wote. Kwa hekima hiyo, inakuwa ni mazoea ya kufanya tafakari na matendo ya huruma.

Tamko la pamoja kutoka mkutano huo linaendelea kusema, hivyo, kwa wote hija ya Kikristo na Buddhist, imesimikwa ndani ya imani ya uhuru, usafishaji wa moyo, huruma na majitoleo ya zawadi ya kujitoa mhanga, kama sharti muhimu katika kujenga amani ya ndani ya mtu binafsi pia kwa ajili ya amani ya kijamii.



Licha ya tofauti zao kiimani , vyote, Maadili ya Wabuddha na maadili ya mafundisho ya Kikristu ni juu ya heshima kwa ajili ya maisha. Hutafuta manufaa msingi kwa wote kupenda wema na huruma. Washiriki walionyesha kwamba, mazungumzo kati ya Mabudha na Wakristo, yalifanyika katika muono wa jinsi ya kukabiliana na changamoto mpya, kama vile tishio kwa maisha ya binadamu, umaskini, njaa, magonjwa, vurugu, vita, n.k ambavyo hudharirisha utakatifu wa maisha ya binadamu na ni sumu ya amani katika jamii ya binadamu.

Washiriki pia walionyesha kutambulia kwamba wana wajibu maalum katika kushughulikia masuala haya. Na hivyo wanaona kuwa hamu ya ushirikiano kwa ajili ya ustawi wa wanadamu,inapaswa kuchipuka kutoka katika kina cha mazoezi ya kiroho. Na ni tu amani ya ndani inayoweza kubadili moyo wa mtu na kumfanya mtu kumwona jirani yake kama ndugu yake wa karibu. Kama kweli tunataka kujenga dunia ya amani, ni muhimu kwamba, sisi tunajiunga na vikosi vya kuelimisha watu, hasa vijana, ili kutafuta amani, ili kuishi kwa amani na kuzifanya sehemu za hatari za kazi kuwa mahali pa amani.

Tamko kutoka mkutano huo linahitimishwa na uthibitisho kwamba , ni tu upendo unaoweza kurejesha au kujenga amani katika mioyo ya watu na kujisimika katikati yetu. Washiriki pia , waliitazama kwa makini njia hii ya amani na kusema kwamba kweli ni ngumu , yenye kuhitaji ujasiri mwingi, uvumilivu , kupania , na kujitolea sadaka. Na walichukulia nafasi hii ya majadiliano kuwa kipaumbele na ishara ya matumaini , na hivyo ni lazima waendelee kutembea katika njia hii kwa pamoja.








All the contents on this site are copyrighted ©.