2013-05-21 11:44:54

Serikali ya Nigeria yatangaza hali ya hatari ili kudhibiti vitendo vya kigaidi!


Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria linasema kwamba, linaendelea kutathmini kwa kina na mapana hali ya hatari iliyotangazwa na Serikali ya Nigeria, kama sehemu ya mbinu mkakati wa kupambana na vitendo vya kigaidi vinavyoendeshwa na Kikundi cha Boko Haram, hususan Kaskazini mwa Nigeria.

Katika mahojiano kati ya Askofu mkuu Ignatius Ayau Kaigama Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria na Shirika la Habari za Kimissionari la FIDES, anasema kwamba, hii si mara ya kwanza kwa Serikali ya Nigeria kutangaza hali ya hatari, lakini bila mafanikio yoyote na matokeo yake ni kuendelea kushamiri kwa vitendo vya kigaidi pamoja na uvunjifu wa misingi ya haki, amani na utulivu.

Kwa upande wake, Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria anasema, Serikali imeamua kuchukua hatua hii kama mkakati wa serikali wa kutaka kupambana na hatimaye kudhibiti vitendo vya kigaidi nchini Nigeria ambavyo vimekuwa ni tishio kubwa la maisha na mali za wananchi wa Nigeria.







All the contents on this site are copyrighted ©.