Mfanyabiashara apanda juu ya Kinara cha Kanisa kuu la Mtakatifu Petro ili kuwashutumu
wanasiasa!
Bwana Marcello Di Fenizio,mfanyabiashara kutoka Italia, siku ya jumatatu alipanda
kwenye Kinara cha Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, akipinga vitendo vya
wanasiasa wa Italia ambavyo vimepelekea hali ngumu ya uchumi pamoja na kutoweka kwa
fursa za ajira nchini Italia. Bwana Fenizio alitandaza bango lake akimwomba Baba Mtakatifu
Francisko kuingilia kati ili kuokoa "Jahazi" la watu wanaokata tamaa.
Akizungumzia
tukio hili, Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Bwana
Fenizio hana jipya, kwani hii si mara ya kwanza kupanda kwenye Kinara cha Kanisa kuu
la Mtakatifu Petro kwa madai dhidi ya wanasiasa. Amekwisha wahi kufanya hivyo dhidi
ya Serikali ya Professa Mario Monti. Madai yake ya sasa anayaelekeza dhidi ya Jumuiya
ya Ulaya.