Shirika la habari za kimissionari la Fides, limetangaza kwamba, habari zake zitapatikana
katika lugha nane, kupitia mpango wa smartphones, unayoitwa "Missio", ambao unaopatikana
bil malipo yaani bure. Huduma hii ilizinduliwa na Papa Fransisko wakati alipokutana
na Wakurugenzi wa Mashirika ya Kipapa ya Kitume ya Kitaifa ya Missioni na pamoja na
wafanyakazi wa Fides, Ijumaa iliyopita , Mei 17 mjini Vatican. Papa Francesco
ilizindua utoaji wa habari huo kwa kubofya juu ya iPad, kama alivyombwa na Padre Andrew
Small, OMI, Mkurugenzi wa Kitaifa wa Mashirika ya Mashirika ya Kipapa ya Misioni nchini
Marekani. Ukurasa huu wa Utume wa uinjilishaji , utakuwa unatoa habari za Kanisa
zilizotolewa kupitia tovuto ya habari za Vatican "news.va", pia kuna picha, sinema
na homilia za Papa, habari ya Kanisa katika ulimwengu na zitakuwa zikitolewa katika
lugha nane. Padre Small katika uzinduzi huo alimwambia Baba Mtakatifu,kwamba wanalenga
kuiweka Injili, ndani ya mfuko wa kila kijana ulimwenguni ,maneno yaliyomgusa Papa
Fransisko wakati akibofya kifungo kilichoandikwa juu yake maneno “sisi ni wainjilishaji”.
Katika siku yake ya kwanza ya kuzinduliwa kwa ukurasa huu, jumla ya watu 1,140
wa kutoka nchi 27 tofauti, waliutembelea ukurasa huo. Padre Small anasema lengo letu
ni kuwasaidia watu kuiona dunia kupitia macho ya imani". Ukurasa huu unapatikana
katika iTunes App na Google Play , ambamo ujumbe wa uinjlishaji, unatolewa katika
lugha nane: Kiingereza, Kihispania, Kiitaliano, Kijerumani, Kifaransa, Kireno, Kichina
na Kiarabu.Karibuni nyote.