Malkia wa Mbingu : zawadi na hazina ya Kanisa..Papa
Jumapili kabla ya kuongoza sala ya Malkia wa Mbingu, Baba Mtakatifu Fransisko, aliwaambia
waamini waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, na
mitaa yake kwamba , wao pia ni zawadi na hazina ya kanisa. Uwanja wa Mtakatifu
Petro ulifurishwa na watu wapatao 200,000, kundi kubwa, wakiwa ni vikundi vipya vya
kitume na jumuiya za Kikanisa vya walei, ambao tangu Jumamosi walimiminika mjini
Roma toka pande mbalimbali za dunia kwa ajili ya kushiriki katika Ibada ya Mkesha
wa Pentekoste kama Papa Francisko, alivyoomba kusali pamoja na vikundi na jumuiya
hizo wakati wa Siku Kuu ya Kushuka kwa Roho Mtakatifu, kama sehemu ya maadhimisho
ya mwaka wa Imani. Siku Kuu ya hii ni kumbukumbu ya kushuka kwa Roho Mtakatifu,
ambayo huadhimishwa kila mwaka kama ishara ya kufunga maadhimisho ya Kipindi cha Pasaka,
na pia ni maadhimisho ya kumbukumbu ya maneno ya Yesu mwenyewe, kwa wafuasi wake,
mimi na kwenda kwa baba lakini hamtakuwa peke bali nitamtuma Roho Mtakatifu kuwa nanyi.
Papa alisema, kama ilivyokuwa kwa mitume wake wakiwa wamekusanyika katika Chumba
cha Juu kusali wakiwa na Mama Maria, Jumapili, ndivyo Roho Mtakatifu alivyoubadili
uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kuwa kama chumba cha wazi cha juu, waamini
kuuishi uzoefu wa kipindi cha mwanzo wa Kanisa, wakiwa wamekusanyika kama watu wa
vipaji mbalimbali, wakifurahia uzuri huu wa kuwa wamoja. Papa alisema hiyo ni kazi
ya Roho Mtakatifu, ambaye daima hutengeneza umoja mpya katika kanisa . Baba Mtakatifu
alivishukuru vyama, vikundi na jumuiya zote za Kikanisa, akisema nyinyi ni zawadi
na hazina ya kanisa . Na kwa namna ya pekee aliwashikuru wote kwa kuja Roma kutoka
pande mbalimbali za dunia. Na kwamba daima wamefanikishwa kwa uweza wa Injili ya Bwana.
Na aliwataka wasiogope , daima wafurahi na kuwa pia wavumilivu, kwa ajili ya umoja
wa Kanisa la Kristu Mfufuka aliye pamoja nao daima na pia aliwaweka chini ya ulinzi
wa Mama Bikira Maria.
Papa pia alikumbuka kutolea sala zake kwa ajili ya maafa
ya mafuriko na maporomoko ya aridhi yaliyotokea huko Emilia Romagna Italia na pia
alitolea sala kwa ajili ya Shirikisho la watu wa kujitolea wa Italia “ONCOLOGY “.
Baada ya hotuba yake Papa akiwa ndani ya gari la wazi aliwazungukia waamini akiwasalimia,
kuwashukuru na kuwabariki.
Na wakati wa kukamilika kwa Ibada ya mIsa kwa ajili
ya Siku Kuu ya Pentecoste, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Ukuzajiwa Uinjlishaji
Mpya, Askofu Mkuu Rino Fisichella, kwa niaba ya vyama vya walei na jumuiya za kikanisa,
alitoa shukurani za dhati kwa Papa Fransisko, kwa homilia yake ya kusisimua na kuwatia
nguvu mpya , za kusonga mbele na utume wao kwa ajili ya Kanisa.