Kwa maji ya ubatizo mnakuwa mwendelezo wa Ukristu nyakati zote ...
Jumapili, katika kukamilisha maadhimisho ya Siku Kuu ya Pentekoste, Rais wa Baraza
la Kipapa kwa ajili ya kukuza Uinjilishaji Mpya, Askofu Mkuu Rino Fischella, alitoa
hotuba fupi ya shukurani kwa niaba ya wanaharakati wote wa Kanisa, vyama vya walei
na jumuiya za kikanisa, ambamo alitaja katika kipindi hiki za siku hizi mbili,Jumamosi
na Jumapili, wameziishi hisia halisi za nguvu mpya iliyotoka juu, kama Bwana Yesu
alivyo ahidi wanafunzi wake. Hivyo wanaharakati kutoka jumuia na vikundi mbalimbali
waliojumuika katika mkusanyiko huu, wao pia kwa maji ya ubatizo, wote wanakuwa ni
mwendelezo wa daima wa imani ya nyakati zote, na katika kuyatolea sadaka maisha katika
utendaji wa kila siku kwa nguvu ya zawadi yake Roho Mtakatifu. Nguvu hii ni uwezo
wa kubadilisha moyo, kubadili namna za kufikiri na kutenda, na kufanya hivyo, ni
uwezo wa kupenda. Kuwa na upendo unaokwenda zaidi ya upeo wetu wenyewe kwa sababu
unatokana kwa Kristo Mfufuka, na kuiingia upya moyoni kama matunda ya Roho Mtakatifu,
mwenye kuongoza katika maisha ya ubinadamu wote kwenye mipaka yake ya kidunia.
Askofu
Mkuu Fisichella , alimshukuru Papa kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa mkesha wa
Pentekoste, ambamo kwa shauku kubwa ya kiinjili, alionyesha njia ya kutenda zaidi
, kwa ajili ya kupata matunda zaidi, katika utume wa walei na jumuia za kikanisa
mbalimbali, duniani. Na aliirejea hotuba ya Papa, ambamo aliwakumbusha daima
kumweka Kristo kuwa kituo kikuu cha rejea, kwa sababu, ni kwa namna hiyo tu Kanisa
hubaki kuwa lenyewe, bila ya kufungwa na nguvu za hofu na mashaka. Na kwamba, utume
wa kuinjilisha kwa ujasiri na uvumilivu, kinyume chake ni lazima kushinikiza ujenzi
wa utamaduni wa kukutana, kuruhusu kuona na kugusa mwili wa Kristo. Kweli, katika
Ekaristi Takatifu Bwana Mfufuka, huwafanya wote kuwa na nguvu mpya ya kurudi katika
jumuiya, ambamo kila mmoja huiishi imani yake. Kwa nguvu za Mwili wa Kristu
chakula chetu, tunapata utambuzi kufahamu dhamira kubwa ya Halifa wa Petro, ambayo
daima anatuhimiza kuwa wanafunzi na mitume wa Bwana Mfufuka, ili kwamba watu wote
ndani yake wapate Maisha mapya. Kuyachukulia Maisha kama zawadi, na Neema, ni utambuzi
wa daima wa kumjua Baba na kuishi katika ushirika naye. Ni hili ndilo msingi wa jamii
ya Kikristo ambamo hupata uzoefu na matunda ya imani. Askofu Mkuu Fisichella
aliendelea kueleza kwamba, katika siku hizi mbili, Papa amewawezesha kuiingia katika
kiini cha mchakato ulioanzishwa wakati wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Katika
hali hii ya mwamko mpya katika Kanisa, kuna hisia kali ya haja ya kushiriki katika
Uinjilishaji Mpya, popote Bwana anapo watuma. Kila mmoja wao anajua kwamba upeo
wa utume ni kuipeleka Injili kwa wote na kuwafanya kuwa chumvi na mwanga kwa watu
wote wake kwa waume.
Askofu Mkuu Fischella alimalizia hotuba yake shukurani
kwa Papa kwa maneno ya Mtume Paulo kwa Wakristo wa Efeso: "nawakabidhi kwa Mungu
na kwa neno la neema yake, ambayo ni uwezo wa kuwajenga ninyi" (Matendo 20:32) . Safari
ni ndefu na yenye changamoto nyingi na ya kuchosha.
Lakini kwa kwa utambuzi
wa hayo, tumeweka tumaini letu katika sala za waamini na maongozi ya Papa , kwa ajili
ya utume huu wa kuwaleta watu kwa Mungu, na pia kwa misaada ya maombezi ya watakatifu
Mwenyeheri Yohane XXIII na Mwenye Heri Yohane Paulo II na pia Mwenyeheri Luigi Novarese,
mtangulizi katika njia hii Kanisa Roma, katika harakati ya ya majitoleo ya mateso.
Asante,
Baba Mtakatifu. Bwana atawazawadia wafuasi wake uthabiti wa imani kwa wote.