2013-05-20 10:52:08

Hoja za Nchi za Nchi za Kiafrika katika Mkutano mkuu wa 66 wa Shirika la Afya Duniani


Bwana Josè Van Dùnem Waziri wa Afya nchini Angola anaongoza ujumbe wa Serikali ya Angola katika mkutano mkuu wa sitini na sita wa Shirika la Afya Duniani unaonza rasmi tarehe 20 hadi 28 Mei 2013 huko mjini Geneva, Uswiss. Nchi 194 wanachama wa Shirika la Afya Duniani zinajadili mikakati ya kuwa na uhakika wa afya kama sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo kimataifa.

Katika mkutano huu, Angola inawakilisha hoja za nchi za Kiafrika kwa kupembua vipaumbele na malengo ya sekta ya afya Barani Afrika. Pamoja na mambo mengine, wajumbe pia wanajadili kuhusu mageuzi makubwa yanayotakiwa kufanyika kwenye Shirika la Afya Duniani, Bajeti kwa mwaka 2014 - 2015; magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza; magonjwa yaliyosahuliwa kutoka Ukanda wa Joto pamoja na huduma ya afya duniani.







All the contents on this site are copyrighted ©.