2013-05-17 15:19:54

Rais Napolitano wa Italia kukutana na kuzungumza na Papa Francisko, hapo tarehe 8 Juni 2013


Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Rais wa Italia Giorgio Napolitano hapo tarehe 8 Juni 2013. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Baba Mtakatifu Francisko na Rais Giorgio Napolitano kukutana rasmi. Itakumbukwa kwamba, Rais Napolitano alikuwa ni kati ya viongozi wakuu wa Serikali na Mashirika ya Kimataifa waliofika mjini Vatican kushuhudia Baba Mtakatifu Francisko akianza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Kama viongozi wengine alipata nafasi ya kusalimiana na Baba Mtakatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro baada ya Maadhimisho ya Misa Takatifu. Hayo yamebaionishwa na Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.