Wakristu toeni jibu la wema kwa mabaya- Papa Fransisiko ahimiza.
Jumapili 12 Mei 2013, Papa Fransiko, ameongoza Ibada ya Misa kwa nia ya kuwataja katika
daraja la Watakatifu, Wenyeheri wafia dini kadhaa ambao ni Mwenye Heri Antonio Primaldo
na wenzake 800 wa Otranto; Mwenye Heri Laura wa Mtakatifu Caterina wa Siena Montoya
y Upegui, Sista na mwanzilishi wa Usharika wa Wamisionari wa Maria Asiyekuwa na Doa
wa Mtakatifu Catherine wa Siena; Mwenye Heri Maria Guadalupe Garcia Zavala, mwanzilishi
mwenza wa Usharika wa Wahudumu wa Mtakatifu Margaret Maria (Alacoque) wa Maskini.
.
Tukio hili la kuwataja Wenye Heri hao kuwa ni Wakatifu, lilipitishwa na
Baraza la Makadinali (Consistory)hapo tarehe 11 Februari 2013, wakati Papa Benedikto
XVI, alipotoa tangazo lake la kihistoria la kujiuzuru kuwa Papa . Watakatifu Mashahidi
wa Otranto ni wa Italy na Watawa Masista wawili ni raia wa Amerika ya Kusini.
Akiwatangaza
Watakatifu hawa , Mashahidi wa Otranto Italia, Sista Laura Montoya Colombia na
Maria Guadalupe GarcĂa Zavala, ametoa wito kwa Wakristu wote kuitangaza Injili kwa
uaminifu si kwa maneno tu lakini hasa kimatendo, kuushuhudia upendo wa Mungu na upendo
Mkristu kwa watu wote kama walivyofanya Mashahidi hawa wa Imani kwa Kristu,ambayo
leo wametajwa kuwa mifano bora ya upendo na maisha ya Kikristo. Ni mifano ya uaminifu
kwa Kristo .
Katika homilia yake , Papa aliyarejea masomo yaliyo somwa akisema
yanatoa wito kwa waamini wote kuwa aminifu kwa Kristo, hata kama ni kuuawa. Na tukio
hii la kuwataja Mashahidi hawa wa Imani kuwa Watakatifu, kunaongeza ukurasa mwingine
mpya katika kitabu cha Maisha ya Watakatifu yanayo paswa kuingwa na wafuasi wote wa
Kristu. Papa alieleza na kurejea hali ya maisha ilivyokuwa katika miaka ya 1480
ambamo watu wa Mashariki ya kati waliishi maisha ya kitisho cha utawala wa Ottoman.
Lakini mashahidi wa Otranto kitisho cha kunyongwa, hakikuondoa imani yao kwa Kristu.
Papa alieleza pia kwa kureja imani ya Mtakatifu Stepahno, akisema ni tu katika
imani, ambamo tunaweza kuona zaidi ya mipaka ya macho yetu binadamu, zaidi ya mipaka
ya maisha ya kidunia, na kuuona ufunuo wa kimbingu na Kristo aliye hai katika mkono
wa kulia wa Baba. Papa aliasa na kutoa wito kwa wabatizwa wote wa kanisa , kutunza
imani yao kama kito cha thamani sana, walichopokea. Ni hazina ya kweli, ambayo daima
kwa uaminifu wetu kwa Bwana, hufanya upya hata katikati ya vikwazo na kutoelewana.
Mungu kamwe hawezi kuacha kutuimarisha na kutupa nguvu na utulivu.