2013-05-12 14:39:56

Askofu MKuu Novarese sasa ni Mwenye Heri.


Jumamosi 11 Mei 2013, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya kuta la hapa Roma, , Katibu wa Vatican, Kardinali Tarcisio Bertone, aliongoza Ibada ya Misa kwa nia ya kumtaja kuwa Mwenye Heri , Askofu Mkuu Luigi Novarese, mzaliwa wa 1914, Italy.

Kwa juhudi zake za kipekee Askofu Mkuu Novarese , alianzisha Umoja wa Wafanyakazi wa Pius wa Ukimya wa Msalaba, pia nyumba ya uuguzi na vituo vya huduma na kozi ya utaalamu kwa ajili ya kuhudumia walemavu na wagonjwa.

Askofu Mkuu Novarese, amepata heshima ya kutajwa kuwa Mwenye Heri, kutokana na utendaji wake unaoonyesha kwamba kweli aliyatumia maisha yake yote kuyatetea maisha ya mtu maskini na mteswa, hata akapata jina la utani “Mtume wa wa wagonjwa”.
Ni Msamaria halisi ya nyakati za zetu na Shahidi wa Injili, aliyemcha Mungu, kupitia wagonjwa na wateswa , kwa sababu aliona ndani yao , kigezo cha maisha ya Kristu Mteswa. Kardinali Tarcisio Bertone , alieleza katika homilia yake , akimtaja kuwa mfano bora wa kuigwa na Wakrtistu wote.
Mwenye Heri "Mtume wa mgonjwa” Luigi Novarese, alizaliwa mwaka 1914 huko Casale Monferrato Italy.








All the contents on this site are copyrighted ©.