2013-05-11 14:43:04

Papa amtembelea Kardinali Javier Lozano Barragàn hospitalini


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi baada ya shughuli zake za kukutana na kuzungumza na watu mbali mbali, Jumamosi, tarehe 11 Mei 2013, alifunga ofisi na kwenda kumtembelea Kardinali Javier Lozano Barragàn, Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Kipapa la wahudumu wa sekta ya afya aliyelazwa kwenye Kliniki ya Pio wa Kumi na moja mjini Roma baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Baba Mtakatifu ametumia fursa hii pia kusalimiana na wafanyakazi wa Hospitali hii na kushangazwa na jinsi ambayo Kardinali Barragàn anavyoyakabili mateso na mahangaiko yake kwa imani na moyo mkuu. Baba Mtakatifu anasema, kwa hakika Kardinali Barragàn ni kielezo cha ushuhuda wa imani. Itakumbukwa kwamba, Kardinali javier Lozano Barragàn kutoka Mexico, hapo tarehe 26 Januari 2013 ametimiza miaka 80 tangu alipozaliwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.