2013-05-11 15:03:42

Furaha ya Mkristu ni zaidi ya kufurahia maisha - asema Papa Fransisko


Furaha ya Kikristu ni hija ya furaha ambamo hatuwezi kubaki tumejifungia ndani kwa ajili yetu wenyewe, vinginevyo tunajiweka katika hatari ya kuwa jamii ya masononeko, uchungu na majonzi. Aidha furaha ya Mkristu, ni zaidi ya kuwa furaha ya kuchekelea tu, ila ni furaha iliyosimikwa katika kina cha kiroho. Na si furaha ya kidunia, kwa sababu msingi wake umesimikwa katika shina la uhakika kwamba Yesu Kristo ni na Mungu na yuko pamoja nasi. .

Papa Fransisko, alifundisha wakati wa Ibada ya Misa aliyoiongoza Katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican ,ibada aliyosaidiana an Askofu Mkuu Bartazar Enrique Porras Cardozo wa Jimbo la Merida , na pia Askofu Mkuu Notker Wolf, Mkuu wa Wabenedkitine, ibada iliyo hudhuriwa pia na wafanyakazi wa Redio Vatican wakiongozwa na Mkurugenzi wa Redio Vatican, Padre Federico Lombardi.

Homilia ya Papa Fransisko, ililenga zaidi aya kutoka Matendo ya Mitume, ambamo mna maelezo kwamba, Mkristo iwe mwanamke au mwanamme, anatakiwa kuwa mtu wa furaha . Ndivyo Yesu anavyotufundisha na pia kanisa hufundisha hivyo.
Papa aliendelea kuitafakari furaha hiyo ya Mkristu akisema, ni zaidi ya furaha ya kawaida kwa kuwa haitokani na sababu za mpito. Hii ni furaha ya kina ya ndani ya moyo, isiyotokana na mafanikio ya kidunia, kama sababu za kiuchumi, fedha na kijamii, lakini hii ni furaha inayotokana na kuuona upeo wa kina wa maisha ya furaha yasiyokwua na mwisho. Ni furaha inayopokelewa kama zawadi kutoka kwa Mungu, inayojazwa ndani mwetu. Ni upako wa Roho kwamba kwa hakika Yesu ni pamoja na sisi na pamoja na Baba. "

Aliendelea kusema, mtu wa furaha, ni mtu wa kujiamini. Ana uhakika kwamba "Yesu ni pamoja na sisi, kwamba Yesu ni pamoja na Baba. Na alihoji kama ni vyema kuifungia zawasi hii ya furaha ndani mwetu daima?.

Na alitoa jibu, "Hapana, kwa sababu kama tutaifungia furahi hii ndani mwetu tu, hatimaye mioyo yetu mioyo yetu itazeeshwa kwa mhemko uliomo ndani na hivyo kuna hatari za kumezwa na masononeko na huzuni na kuwa na hofu na uzembe, na kushindwa kuitangaza furaha ya Injili na hili kiroho si afya njema. .Wakristu ni lazima kuinua kisingino na kuwenda kuitangaza furaha ya Injili kwa kila binadamu. Nikuifunua mioyo wazi kwa kila mtu ili aweze kuiona furaha hii kamili..
Furaha hii, ni nguvu ya hija, ni zawadi inayotusindikia katika kuitembea njia ya maisha, tunapoi tembea na Yesu, kuhubiri, na kuwaleta wote waliolemewa na maisha uchoyo, ubinafisi, ulafi, ufisadi, ufuska na dhambi nyingine nyingi kwa Yesu. Ni furaha ya kuwakaribu ndani ya Kanisa wote, ili pia wayaone maisha yao kwa mtazamo wa upeo wa macho ya Kikristu.

Furaha ni Hija, Papa Fransisko amesisitiza, Mkristo anapo imba kwa furaha, kinakuw ani kitendo cha kuishuhudia furaha yake inayotoka ndani moyoni mwake na kuioneysha wazi katika njia ya maisha yake ya kuelekea Mbinguni. Furaha ni nguvu ya Mkristu katika hija yake , na ni zawadi inayotolewa kwa Ukarimu na Kristu Mwenyewe pamoja na Roho Mtakatifu.








All the contents on this site are copyrighted ©.