Majeshi kutoka Kusini mwa Afrika kuimarisha amani, Mashariki mwa DRC
Afrika ya Kusini, Tanzania na Malawi ni kati ya nchi ambazo zinachangia Askari watakaoshiriki
kulinda amani kwenye mpaka kati ya DRC, Rwanda na Uganda, maeneo ambayo kwa miezi
ya hivi karibuni yamekuwa ni uwanja wa vita unaodhibitiwa na Kikosi cha Waasi cha
M23 kinachoungwa mkono na Serikali ya Rwanda na Uganda, ingawa Serikali zote mbili
zimekwisha kanusha tuhuma hizi.
Hivi karibuni Kikosi cha M23 kilitoa vitisho
kwa Serikali ya Tanzania na kujibiwa kwamba, Tanzania ni moto wa kuotea mbali, ikithubutu,
itakiona cha mtema kuni! Afrika ya Kusini ambayo kwa sasa ina uchumi mzuri inaonekana
itachangia zaidi katika masuala ya vifaa vya kijeshi kama njia ya kuimarisha amani
huko Mashariki mwa DRC.