2013-05-09 08:23:24

Radio Waamini Kenya inaadhimisha Kumbu kumbu ya Miaka 10 tangu ilipoanzishwa


Askofu Martini Kivuva wa Jimbo Katoliki la Machakosi Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Miaka 10 tangu Radio Waamini inayomilikiwa na kuendeshwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya ilipozinduliwa. Kilele cha Maadhimisho hayo ni hapo tarehe 12 Mei 2013 sanjari na Maadhimisho ya Siku ya Upashanaji Habari Ulimwenguni kwa mwaka 2013.

Tamasha la Vyombo vya Habari nchini Kenya limeandaliwa na wadau wa vyombo vya Mawasiliano ya Jamii ndani ya Kanisa Katoliki nchini Kenya. Ndani ya viunga vya Radio Vatican tunaye Padre Joseph G. Healey, MM, anayefanya utume wake nchini Kenya akizungumzia umuhimu wa mitandao ya Kijamii kama majukwaa mapya ya Uinjilishaji Mpya. RealAudioMP3







All the contents on this site are copyrighted ©.