2013-05-09 15:24:39

Mama Wakuu: Jengeni Furaha ya Kimama katika Kanisa--Papa


Jumanne Asubuhi, ukumbi wa Paulo wa V1, ulipambwa kwa sura za Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa ya Kike, wapatao zaidi ya 800, ambao walikuwa Roma kuhudhuria Mkutano wao. Mama Wakuu hao walitoka katika Mataifa 75 wakiwakilisha Watawa wa Kike wapatao zaidi ya laki saba(700,000) waliotawanyika duniani kote. Mkutano wa Mama Wakuu, uliokuwa ukiongozwa na Mada : “Huduma ya Utawala kwa mujibu wa Injili “, ulifungwa Jumanne kwa kukutana na Papa Fransisko katika Ukumbi wa Paulo V1.
Papa Fransisko akiwahutubia Mama Wakuu hao aliwahimiza kutenda utume wao kwa furaha kuu kwa kuwa ni haki na vyema kumfuata Kristu.
Papa aliwakumbusha kwamba ni Kristu mwenyewe aliyewaita kuyafuata maisha yaliyo wekwa wakfu na hii ina maana, daima ni kuandamana katika msafara wa maisha ya Kikristu na Injili yake na juu ya mapenzi ya Mungu kwa ajili ya utukufu wa Mungu na binadamu wote, kama alivyosema Mtakatifu Paulo: “si mimi tena ninayeishi bali ni Kristo anayeishi ndani yangu"

Papa aeliendelea kufafanua juu ya maisha ya kitawa akisema, ni maisha yanayoongoza katika njia ya imani na uchaji kwa Mungu na huduma ya Bwana kwa ndugu zetu, waume kwa wake, kupitia misingi mitatu ya kitawa, ambayo ni utii, umaskini na usafi wa Roho.

Ni kusafiri katika njia ya utiii wa kusikiliza mapenzi ya Mungu, kwa kishindo kinachotoka kwa Roho Mtakatifu na Kanisa, ni kukubali kuwa na utii hasa katika hatua za utendaji, kuptia huduma ya upatanishi.

Papa aliendelea kuzungumzia mahusiano ya utawala na utii akisema kwamba, inafaa katika muktadha mpana wa huduma ya Kanisa ambao huwezeshwa ushirikiano katika utendaji wa pamoja na mapatano, yanayoandamana na hamu ya kuwa maskini, nyenye kuishinda roho ya ubinafsi wa kujilimbikizia mali, katika mantiki ya Injili, ambayo inatufundisha kutegemea kudra ya Mungu, kama ishara kwa Kanisa lote kwamba, Ufalme wa Mungu haujengwi na mali za binadamu, lakini kimsingi ni nguvu na neema ya Bwana, ambaye hufanya kazi kupitia udhaifu wetu.

Na umaskini hufundisha kwamba, mshikamano, kugawana na upendo pia huonyesha unyenyekevu na kuridhika kwa furaha, ameonya Papa na kuongeza tamaa ya vitu huweka giza katika maana ya kweli ya maisha ya Mkristu.

Katika Umaskini tunajifunza kuwa wanyenyekevu katika jinsi ya kuwahudumia wengine waliopungukiwa, wagonjwa na wale wote ambao malisho ya maisha yako hatarini. Na umaskini wa kinadharia hauna maana yoyote , lakini unatakiwa kweli kuuishi umasikini kama Yesu alivyouishi wakati akiwa hapa dunaini kama binadamu , aliishi katika hali ya umaskini na unyenyekevu wa kuhudumia wahitaji maskini, wagonjwa na waliodhaifu zaidi kama watoto ... "

Kisha Papa alizumgumzia kipengere cha usafi wa moyo, akisema, ni karama ya thamani sana, ya majitolea huru kwa Mungu na kwa wengine, kwa upole, huruma, ukaribu kwa Kristo. Na aliwaasi karama hiyo iwasaide kuzaa watoto wengi wa kiroho kwa kanisa. Na kwamba wao si wajane. Wao ni Mama, na Ishara ya Mama Bikira Maria Kama wa Kanisa. Ni vingumu kuelewa inavyoweza kuwa Kanisa, uwepo wa Kanisa bila huduma ya kimama. Hivyo wao ni nembo ya Maria na Kanisa.


Na Kuhusu dhana ya mamlaka na huduma, vipengere vilivyokuw akiini cha majadiliano ya mkutano wao Papa alikumbusha hatari ya fikira za kibinadamu ambazo mara nyingi huelekeza kwamba kuwa mtawala ni kumiliki , kuwa na mamlaka na kulenga katiak mafanikio tu. Lakini kumbe , kwa ajili ya mamlaka ya Mungu, daima huwa ni huduma katika unyenyekevu na upendo ":

Papa aliwaonya na kuwarejesha katika matukio mengi na fikiria haribifu, ambazo zimewanywa naviongozi wa kanisa wake kwa waume , na kusabbisha watu kulikimbia kanisa la Kristu. Viongozi hao wabovu, humezwa na kishawishi cha kukumbatia ubinafsi na choyo , na kutaka kuifanya huduma ya uongozi kama chombo cha kupandia ngazi kwa maslahi yao wenyewe na matarajio ya binafsi. Papa ameutaja udhaifu huo kwamba, hufanya madhara makubwa kwa Kanisa! "

Hatimaye, Papa aliwataka Mama wakuu kuuishi wito wao katika wakfu na kuziishi karama za kikanisa wakijisikia daima ni wana wapendwa wa Kanisa na daima wako kwa ajili ya kutangaza Injili na ushuhuda kwa Injili "ni kamwe si utendaji wa kipeke au kundi moja peke lakini ni Kujisikia ndani ya Kanisa kwamba , kwa Ubatizo tuliopokea wabatizwa wote huwa kitu kimoja katika kujieleza kwa uaminifu katika ushirika na Maaskofu na Halifa wa Petro, Askofu wa Roma, ishara inayoonekana ya umoja. "

Papa alimalizia na mshangao kwa wanaofikiri kuishi na Yesu bila Kanisa, kumfuata Yesu nje ya kanisa, kumpenda Yesu nje ya Kanisa. Kwa kifupi kiini cha Kristo na Injili yake, mamlaka yanakuwa ni huduma ya upendo, na kujisikia kuwa ndani ya Kanisa Mama."








All the contents on this site are copyrighted ©.