2013-05-08 15:41:01

Ubinafsi hauwezi kuleta maendeleo kijamii.


Maendeleo ya kweli ya binadamu hayawezi kufanikishwa na ubinafsi...
Ni maelezo yaliyomo katika barua ya tatu ya Patriaki Moraglia kwa Makanisa ya Venezia kwa ajili ya mwaka wa Imani. Amesema, muonekano wa mtu, ni kipimo cha maendeleo ya kweli ya binadamu. Na hili ni msingi wa Mafundisho ya kijamii ya Kanisa, kama ilivyo ainishwa na waanzilishi wa mafundisho hayo , Mababa wa Kanisa katika Hati yao inayo timiza miaka 50 ya uwepo wake.

Patriaki Fransisko Moraglio , ametoa Waraka wa tatu wa Kichungaji kwa Kaniia la Venice, kama mchango wake, katika yale yanayotakiwa kuzingatiwa na Wakristu, wakati wa maadhimisho ya mwaka huu wa imani, katika tafakari za yale yaliyopendekezwa mwezi Octoba mwaka jana, wakati wa kuzinduliwa kwa mwaka wa Imani, juu ya Madambiu “Imani ya Kikristu katika mtazamo wa kuenea kwa malimwengu”.

Waraka huo mpya, unasisitiza umuhimu wa kugundua na kujifunza mafundisho ya kijamii ya Kanisa, ambayo yanatoa sura mpya juu ya ufunuo wa kimungu na hoja za kumweka mtu kuwa ndiye kiini cha maendeleo katika juhudi zote za utendaji wa jamii.

Waraka wa Patriaki Moraglia, umerudia kutaja na kusisitiza juu ya Kanuni msingi ya kwanza , katika utendaji wote , kwamba ni utakatifu wa maisha ya mtu, hadhi ya ubinadamu wa mtu, kwamba, hadhi ya utu wake ndiyo msingi wa utendaji wote mzuri wa kijamii , umoja na mshikamano wote wa binadamu.

Na hivyo mtu hapaswi kumezwa na fikira za kudhani au kujiona kama ni yeye binafsi anajitosheleza, lakini daima azingatie kwamba, ni mmoja lakini katika muungano na wengine. Ni mtu mmoja lakini katika uhusiano na wengine , na hakuna kinachoweza kutengua hilo.

Hivyo, hakuna maendeleo ya kweli ya binadamu, kama maendeleo hayo yanafanywa katika misingi ya utamaduni wa ubinafsi. Jamii ya binadamu inapaswa kuishi katika lengo la mtu kwa manufaa ya wengine. Na ndiyo njia ya kutembea nayo katika tafakari za mwaka huu wa Imani








All the contents on this site are copyrighted ©.