2013-05-08 07:34:30

Makleri na watawa wanavyochakarika kutumia mitandao ya kijamii katika Uinjilishaji mpya!


Jimbo kuu la Roma linajiandaa kikamilifu kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya 47 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni ambayo kwa mwaka huu, itaadhimishwa kwenye Siku kuu ya Bwana Kupaa Mbinguni hapo tarehe 12 Mei 2013 kwa kuongozwa na kauli mbiu “Mitandao ya kijamii: milango ya ukweli na imani”.

Idara ya Mawasiliano ya Jimbo kuu la Roma kwa kushirikiana na wadau mbali mbali katika sekta ya mawasiliano ya Jamii inasema, hapo tarehe 9 Mei 2013 kutafanyika semina ya siku moja itakayokuwa ni fursa kwa wadau wa sekta ya mawasiliano ya Jamii kutafakari kuhusu ujumbe wa Siku ya 47 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni uliotolewa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita.

Washiriki watafahamishwa kuhusu tafiti zilizofanywa kuhusu Kanisa na Mitandao ya Kijamii na kwa namna ya pekee jinsi ambavyo Makleri na Watawa katika mchakato wa Uinjilishaji mpya wanavyochakarika kutumia mitandao ya Kijamii.

Mada hii itawasilishwa na Professa Rita Marchetti kutoka Chuo Kikuu cha Perugia, Italia. Ni utafiti ambao umefanywa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Milano na Chuo Kikuu cha Perugia nchini Italia.








All the contents on this site are copyrighted ©.