2013-05-07 15:27:01

Uteuzi...Majimbo ya Kokstad na Kabungo yapata Maaskofu


Baba Mtakatifu Fransisko amemteua Padre Zolile Peter Mpambani , kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kokstad, Afrika Kusini.

Askofu Mteule Zolile Peter Mpambani S.C.I, alizaliwa 20 Februari 1957 huko Umlamli katika Jimbo la Aliwal. Na alijiunga na Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu Januari 28, 1982. Amehitimu ktiak masomo ya Filosofia na teolojia katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Joseph ya Cedaral. Na alipadirishwa tarehe 25 April 1987.
Hadi kuteuliwa kwke alikuwa Vika Mkuu wa Parokia katika Jimbo la Aliwal. Pia Februari aliteuliwa kuwa Mkuu wa Kijimbo wa shirika la Moyo Mtakatifu, Kanda ya Afrika Kusini.
Jimbo la Kokstad lilizinduliwa mwaka 1951 kama sehemu ya Jimo Kuu la Durban , Lina wakazi 1,809,000 kati yao 85,000ni Wakarìtoliki wanaohudumiwa chini ya Parokia 16, zinazo ongozwa na Mapadre 21 wakiwa wa jimbo 8 na 13 wa mashirika ya kitawa,. Kuna Mafrateli 16, Masista 44 na waseminaristi watano .
Kiti cha Askofu cha Jimbo la Kokstad kilibakiwazi Januari 31 baada ya Askofu jimbo hilo kuhamishiwa katika Jimbo Kuu la Pretoria.

Aidha Papa ameteua Askofu wa Jimbo la Kibungo Rwanda
Baba Mtakatifu amemteua Padre Antoine Kambanda , Gombera wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Charles ya Nyakibanda Butare, kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kibungo Rwanda.

Askofu Mteule alizaliwa 10 Novemba 1958 jimboni Kigali. Wazazi wake wote wawili waliuawa wakati wa vita vya mwaka 1994. Alijipatia elimu ya awali nchini Burundi na Uganda na masomo ya sekondari nchini Kenya. Alisoma masomo ya filosofia na teolojia nchini Rwanda na kukamilisha elimu ya teolojia katika seminari Kuu ya Nyakibanda jimboni Butare.

Alipadirishwa Septemba 8 1990 na Mwenye Heri Papa Yohane Paulo 11, wakati akitembela Rwanda. Na alifanywa kuwa Gombera wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Charles ya Nyakibanda mwaka 2006. Kiti cha Askofu katika jimbo la Kibungo kilibaki wazi tangu mwaka 2010, baada ya Askofu wa jimbo hilo kustafu kwa mujibu wa sheria ya Kanisa 401/2..








All the contents on this site are copyrighted ©.