Ushirika
wa Kitume, sala na Uchaji: Mama Yetu wa Quintiliolo. |
Jumapili iliyopita, Katika Maadhimisho ya mwaka wa Imani
, Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ulipambwa na maelfu ya wawakilishi kutoka
Mashirika na vyama vya kitume na Uchaji , walioitolea Jumapili hiyo kuwa ni Siku
Maalum katika maadhimisho ya mwaka wa Imani, kwa ajili ya maisha yao ya usharika
wa utume sala na Uchaji. Tukio hili walilianza tarehe 3 May, chini
ya Mada : tangu katika mitaa ya dunia, shuhuda za imani , vyama vya kitume sala na
uchaji , katika hija kwenye kaburi la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya Uinjilishaji
mpya. Mahujaji hao walitembelea Kaburi la Mtakatifu Petro, mapema siku ya Jumamosi
. Mapema , Askofu Mkuu
Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Ukuzaji w a Uinjilishaji Mpya,
aliizungumzia hija hii ,akisema, waamini zaidi 50, 000, walitarajiwa kushiriki katika
hija hii hapo May 5 . Na kwamba ulikuwa ni wakati kwa waamini hao, kutafakari kwa
namna nyepesi juu ya imani na uchaji uliosimikwa kwa kina, katika maisha ya kuziishi
alama za kuonekana, kama kaburi la Mtakatifu Petro, zenye kukumbusha imani ya watu
wa karne zilizopita na hivyo kuwa ushuhuda katika utamaduni wa imani, zenye kuhimiza
na kutupatia mwamko na hamu ya kuuishi imani kwa shauku zaidi. Askofu Mkuu Fischella alizitaja jumuiya hizi kuwa ni shuhuda hai mbalimbali
kutoka kwa watu wa lika na hali mbalimbali wanaotafuta kuiimarisha na kuiishi imani
yao si kwa maneno tu lakini katika utendaji wa maisha ya kila siku, katika umoja kamili
wa kidini na kanisa. Kati ya wanajumuiya waliokuwepo, ni kutoka
Roma, ambao waliwasilisha mchoro maalum wa karne ya 13 unaomwonyesha Mama Bikira
Maria na Mtoto wake, ili mchoro huo, upate mastahili ya kuwekwa Altareni. Sanamu hiyo
iliyochorwa katika kipande cha ubao , na hujulikana kwa jina la Mama Yetu Asiyepungukiwa,
wa Mazao, pia inaitwa kwa jina jingine, Mama Yetu wa Quintiliolo. |
All the contents on this site are copyrighted ©. |