Italia yamlilia Giulio Andreotti na hali mchanganyiko
Italia inamlilia Giulio Andreotti., aliyekuwa senata wa maisha, aliyefariki Jumatatu
06 May 2013, asubuhi, nyumbani kwake Roma, akiwa na umri wa miaka 94.
Mwana
habari Alessandro Guarasci wa Radio Vatican anabainisha kwamba, kwa miaka 40, Andreotti
alikuwa mmoja wa nembo ya siasa Italia. Ingawa hakupendwa na wengi, lakini ameacha
mengi ya kukumbukwa, mojawapo ikiwa ni mwanasiasa mkongwe aliyechanguliwa kuingia
bungeni akiwa na umri mdogo wa miaka 27 tu . Na aliongoza serikali ya Italia kama
Waziri Mkuu kwa mara 7, na kuwa mjumbe wa bunge kwa miaka sitini na sita.
Mazishi
ya mwanasiasa huyu mashuhuri Italia , yanafanyika katika hali ya faragha kulingana
na matakwa yake. Katika maisha yake ya kisiasa, alikabiliwa na tuhuma mbalimbali,ikiwemo
kuhusishwa na kikundi haramu za mafia, tuhuma alizokanusha vikali.
Kardinali
Camillo Ruini, akimwelezea Marehemu Giulio Andreotti, amerejesha kumbukumbu zake
za zamani, akiwa Katibu wa Baraza la Maaskofu la Italia, alipokutana binafsi na
Andreotti mwaka 1986, kwmba , alivutwa na hisia na hekima za Andreotti, ambaye licha
ya kuwa mtu mcheshi na mtanashati, pia alijaliwa busara na hekima , asiyeficha maadili
ya Kikristo, wala kuificha imani yake Katoliki. Na alikuwa mtu mwerevu aliyejua vyema
mbinu za kusawazisha marumbano katika utendaji wa taasisi za kisiasa na imani yake
kama Mkristu .
Na rais wa CEI, Kardinali Angelo Bagnasco ametaja umuhimu
wa Andreotti kwa Jamhuri ya Italia, kwa kuonyesha matumaini yake kwamba, Italia itaangalia
historia ya maisha ya Andreotti na kuyachukua yote yaliyo mema kwa ajili ya manufaa
ya taifa la Italia. .