2013-05-07 11:31:19

Changamoto pevu kwa vikosi vya ulinzi na usalama Barani Afrika!


Vyombo vya ulinzi na usalama Barani Afrika vinakabiliwa na changamoto pevu inayoendelea kuongezeka siku hadi siku: ya wimbi la biashara haramu ya binadamu, biashara na matumizi haramu ya dawa za kulevya; vitendo vya kigaidi na vile vya jinai vinavyofanywa kwenye mitandao bila kusahau utakatishaji wa fedha unaofanywa na makundi ya kijasusi Barani Afrika ili kugharimia vita, migogoro na kinzani za kijamii. Kuna watu wenye uchu wa kutaka kukwapua rasilimali ya Bara la Afrika kwa ajili ya mafao yao binafsi.

Ni changamoto ambayo imetolewa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe siku ya Jumatatu, tatehe 6 Mei 2013 wakati alipokuwa anafungua mkutano wa kamati za ulinzi na usalama kutoka katika nchi 49 za Kiafrika. Tangu mwaka 1990 migogoro ya kivita na kinzani za kijamii zipatazo 20 zimetumika kwa ajili ya kuchunguza rasilimali na utajiri wa Bara la Afrika kwa ajili ya mafao ya watu wa nje.







All the contents on this site are copyrighted ©.