2013-05-06 10:52:18

Papa Fransisko : Kila binadamu ana wajibika kulinda na kutetea hadhi ya binadamu.


Baba Mtakatifu Fransisko, Jumapili , wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu, alisali sala hiyo pamoja na maelfu ya mahujaji na wageni walikusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro . Katika mtazamo wa Mwaka wa Imani, hotuba yake ya kabla ya sala, ilizungumzia uwepo wa kiroho wa Bikira Maria, aliye hai katikati yetu.
Alisema maadhisho ya Siku hii ya kujitolea ya vyama vya kitume na sala na Uchaji Mpya, upendo kwa Maria, unajionyesha kuwa ni moja ya tabia maalum ya utawa, katika kuwa na nguvu, hisia na maamuzi thabiti .
Papa Francis alitoa mwaliko kwa wote, kuitafakari hija ya Maria, aliyeianza njia ya kutembea na Yesu, Mwana pekee wa Mungu, na hivyo kuwa mwanga wa kutuongoza sisi sote katika njia hii ya imani."

Papa Francisko pia aliutumia muda huo , kutoa slaam zake za matashi mema kwa Wakristo wote wanaofuata kalenda ya Juliana, ambao Jumapili walifikia kiilele cha Maadhimsho ya Siku Kuu ya Pasaka. Katika salaam hizo,alisema, anapenda kuungana nao katika kuitangaza habari jena kwamba,Kristo amefufuka" . Na hasa wale wanaoiadhimisha siku kuu ya Pasaka katika hali za majaribu na mateso. Na aliomba Roho Mtakatifu , awaongoze katika mashauri na faraja na katika njia ya amani na maridhiano.

Pia alizungumzia juu ya tukio la Jumamosi la kutajwa Mwenye Heri, Francisca de Paula De Yesu, anayeitwa "Nha Chica." Na aliionyesha kufurahia kuungana na Kanisa la Brazil, kuifurahia nuru hii mpya ya mwanafunzi wa Bwana."

Na aliyasalimu makundi mbalimbali ya vyama na mashirika kitume pamoja na makundi ya kiparokia ya makundi na familia. Na aliwakumbuka watoto walioathirika na wanaoendela kuathirika Vurugu mbalimbali, akisema ni mateso makubwa kwa watoto, na hata watu wazima na hivyo akatoa ombi lake kwa kila mtu, kulinda na kutetea ubinadamu wa watu wote , lakini hasa watoto, wanaoishi miongoni mwa mazingira magumu zaidi.

Katika salamu zake za mwisho, Papa Francis inawaombea faraja za Bwana Mteswa na Mufufuka, wale wanaosumbuliwa na shinikizo la damu na kwa familia zao.










All the contents on this site are copyrighted ©.