2013-05-06 10:37:18

Hali ya usalama bado si shwari Bangui


Kikosi cha Waasi cha Seleka hivi karibuni kilichoma zaidi ya nyumba 400 na kupelekea watu 9 kupoteza maisha yao pamoja na kunajisi Kanisa kwenye Kijiji cha Ouango, Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati. Inasemekana kikundi hiki kilichosababisha maafa makubwa kiasi ni kutoka nje ya nchi.

Watu wengi wanaendelea kupoteza matumaini na kwamba, jitihada za kuanzisha mchakato wa majadiliano ya kidini kati ya Wakristo na Waislam katika eneo hili bado zinakwama. Mgogoro wa kivita nchini humo unaendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Watoto wanaendelea kupelekwa mstari wa mbele katika mapambano haya, jambo ambalo linawanyima watoto hao haki zao msingi.







All the contents on this site are copyrighted ©.