2013-05-02 14:42:23

Ibueni mbinu mkakati wa kutengeneza fursa za ajira!


Baba Mtakatifu Francisko wakati huu Jumuiya ya Kimataifa inapoendelea kuadhimisha Siku kuu ya Wafanyakazi anapenda kuyaelekeza mawazo yake kwa wote ambao hawana fursa za ajira; tatizo ambalo wakati mwingine linachangiwa na ubinafsi na tamaa ya kupata faida kubwa kwa gharama yoyote ile! Huu ni ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa siku ya Alhamis, tarehe 2 Mei 2013.

Kwa upande wake, Sekretarieti ya Vatican inasema, Baba Mtakatifu Francisko anawachangamotisha wale wote wenye dhamana katika ngazi mbali mbali za maisha ya kijamii kuchukua hatua za makusudi zitakazosaidia upatikanaji wa fursa za ajira ili kutoa matumaini kwa wafanyakazi.







All the contents on this site are copyrighted ©.