2013-05-01 11:28:28

Afya ya Mzee Madiba yasababisha gumzo Afrika ya Kusini!


Chama cha ANC cha Afrika ya Kusini kimekanusha habari zilizovumishwa na mitandao ya kijamii iliyokuwa inaushutumu uongozi wa juu wa Chama cha ANC kwa kupiga picha na Mzee Nelson Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambaye kwa sasa anaonekana kwamba, amedhohofu sana kama kampeni ya kutaka kujijenga kisiasa.

ANC inasema picha zilizopigwa na hatimaye kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii inataka kuwashirikisha watu hali halisi ya maisha ya Mzee Nelson Mandela kwa sasa na wala si kutaka kumdharirisha kama wanavyodai baadhi ya watu ndani na nje ya Afrika ya Kusini. Mzee Madiba kwa miezi ya hivi karibuni hali yake imeendelea kudhohofu kiasi cha kulazimika mara kadhaa kulazwa Hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.







All the contents on this site are copyrighted ©.