2013-04-27 14:56:31

Wawakilishi kutoka Afrika katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani


Baba Mtakatifu Francisko, katika Maadhimisho ya Jumapili ya tano ya Kipindi cha Pasaka, tarehe 28 Aprili 2013 anatarajia kuwaimarisha waamini 44 kwa Sakramenti ya Kipaimara, katika Ibada ya Misa Takatifu itakayofanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kama sehemu ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita na kuridhiwa na Papa Francisko.

Wakristo wanaoimarishwa kwa Sakramenti ya Kipaimara ni kama ifuatavyo: Bara la Afrika lina wawakilishi 7; Amerika 8; Asia 9; 19 kutoka Ulaya na 1 anatoka Oceania. Taarifa zinabainisha kwamba, Libania Maria Silva mwenye umri wa miaka 55 ni kati ya Wakristo wenye umri mkubwa zaidi ambao wamepata bahari ya kuimarishwa na Baba Mtakatifu Francisko. Yeye anatoka Capoverde. Wengine kutoka Barani Afrika ni kama ifuatavyo:
2. Risely Cilente Oliviera Lopez, Capoverde: umri wa miaka 25.
3. Nelly Mundambu Masala; Congo Brazzaville, umri wa miaka 12.
4. Angele Mulibinge Kaj; Congo Brazzaville, Umri miaka 12.
5. Miraniaina Lèa Fanjanirina, Madagascar; umri miaka 21.
6. Yakubu Fatima, Nigeria, umri miaka 16.
7. Aniakor Johnbosco, Nigeria, umri miaka 11.

Ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, hawa ndio wawakilishi kutoka Bara la Afrika katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili tarehe 28 Aprili 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.