2013-04-27 07:44:23

Vijana msifiche karama zenu!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mtandao wa kijamii al maarufu kama twitter anawaalika vijana kwa namna ya pekee kutofisha karama ambazo wamekirimiwa na Mwenyezi Mungu. Anawaalika kutoogopa kuota ndoto ya mambo makubwa!

Ujumbe huu wa Baba Mtakatifu Francisko unakuja wakati huu ambapo kuna bahari ya vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaoshiriki katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani hapa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Jumapili, tarehe 28 Aprili 2013, Baba Mtakatifu atatoa Sakramenti ya Kipaimara kwa Wakristo 44 ambao, watakuwa tayari kumshuhudia Kristo kwa maneno, lakini zaidi kwa njia ya matendo yao.

Tukio hili ambalo linaendelea kuwashangaza wakazi wa Roma kutokana na wingi wa vijana waliopo kwa sasa, linawajumuisha vijana ambao wamepokea Sakramenti ya Kipaimara au wanatarajia kupokea Sakramenti hii katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani.







All the contents on this site are copyrighted ©.