Ofisi ya Kipapa inayohusika na Ibada za Kiliturujia za Papa, hivi karibuni imezindua
ukurasa wake ndani ya twitter kwa jina la @ ucepo. Ukurasa huu uliozinduliwa siku
mbili zilizopita , ambao awali ulikuwa ukitumia ukurasa wa @pontifex, kwa lugha
ya kiitalino, tayari una wanachama zaidi ya 350. Ukurasa huu mpya , unaifanya
twitter kuwa na kurasa tano kwa ajili ya kufanikisha utoaji wa habari za Vatican,
Mitaguso ya kiliturujia , na pia sasa kwa ajili ya ajili ya Ibada ya Misa za Kipapa
ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kama ilivyo ibada itakayofanyika Jumapili
hii, 28 April, ambamo Papa , atatoa Sakramenti ya kipaimara kwa makumi kadhaa ya
waamini.
Kuzinduliwa kwa @ UCEPO, kunaongeza uwezekano wa mawasiliano, kupitia
uanachama wa Twitter, kama ilivyokuwa rahisi sasa kupata habari na orodha ya idara
za Vatican. Yatosha kuandika @TerzaLoggia, au @ proLaicis ofisi ya Baraza la Kipapa
kwa ajili ya Walei, @ PCCS_VA, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano ya Jamii.
na gazeti la kila siku la Vatican L'Osservatore Romano, ambalo linapatikana kirahisi
ndani ya Twitter, kw lugha ya kiitalino ni @ oss_romano, na Kiingereza, ni @ LOsservatore_USA.
Na pia inafaa kukumbuka kwamba, @ newsva,ni huduma katika lugha kadhaa zilizotolewa
na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano ya kijamii na pia huweza kukusanya habari
kutoka vyombo vya habari vikuu vya Vatican.