2013-04-27 15:53:48

Siku ya Kimataifa kuenzi Maisha itaongozwa na Kaulimbiu: Tunasadiki Utakatifu wa Maisha


Tuna Imani na Utakatifu wa Maisha ni kaulimbiu itakayoongoza adhimisho la Siku ya Kimataifa kwa ajili ya Injili ya Maisha (Evangelium Vitae), kama itakavyoandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjiishaji mpya.

Baraza hilo limeandaa mkutano Roma tarehe 15 na 16 Juni 2013, unaotajwa kuwa wa muhimu, na kama nafasi kwa waaamini kutoka pande zote za dunia , kwa pamoja, kuungana na Baba Mtakatifu Francisko , kama kundi moja , kushuhudia thamani takatifu ya maisha: iwe kwa wazee, wagonjwa, walioko kufani na hata wale ambao bado kuzaliw au wale wote wanaoteswa daima maradhi ya kimwili na taabu zingine.

Inatumainiwa kwamba , tukio hili litakuwa ni fursa ya kuenzi, kuimarisha na kutia moyo, wale wote ambao kwa ukarimu na unyenyekevu wameyatolea maisha yao yote bila ya kujibakiza, kufuata nyanyo za Mchungaji mwema, Yesu Kristu, kwa ajili ya kuwahudumia kihali, kisaikolojia na kiroho, wazee, walemavu, wagonjwa, wasiozaliwa bado, walioko kufani na wanao kabilwa na mateso mengine.

Ni matumaini ya waandaaji wa tukio hili kwamba, watu wengi watakaokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya adhimisho la Siku ya Kimataifa ya Utakatifu wa Maisha, itakuwa ni ushuhuda wa nguvu toka Roma kwa dunia, ukiieleza dunia yote, ukweli wa ujumbe wa Kuokoa wa Yesu: "Nimekuja ili wawe na uzima, tena uzima tele(Yn 10:10).

Habari zaidi juu ya tukio hli zinapatikani katika ukurasa wa mtandano WWW.ANNUSFIDEI.VA.








All the contents on this site are copyrighted ©.