Papa Francisko anasali kwa ajili ya kuwaombea waliokumbwa na ajali mjini Dhaka, Bangaladesh
Baba Mtakatifu Francisko anawaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii maarufu kama
twitter kuungana naye kusali kwa ajili ya kuwaombea watu waliopatwa na ajali ya kuangukiwa
jengo mjini Dhaka, Bangaladesh, ili Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji na kuziimarisha
familia zilizoguswa na msiba huu mkubwa.
Hivi karibuni jengo la kiwanda cha
kutengeneza nguo mjini Dhaka liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 332 na wengi
kujeruhiswa vibaya. Jeshi la Polisi nchini Bangaladesh limekwisha watia mbaroni wakurugenzi
wakuu wawili wa kiwanda hicho kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Idadi ya watu waliofariki
inaweza kuongezeka maradufu kwani inasemekana kwamba, kuna watu ambao bado wamefukiwa
na kifusi cha jengo lililoporomoka.