2013-04-26 10:07:39

Mwezi mmoja umepita tangu mapinduzi yatokee Bangui!


Ulinzi na usalama; amani na utulivu ni kati ya ndoto ambazo wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya kati wanatamani kwa siku kadhaa sasa tangu Kikosi cha Waasi wa Seleka ilipojitwalia madaraka na mji mkuu wa Bangui, ukaangukia mikononi mwao!

Hali bado ni tete, kwani watu wengi wanaendelea kulalamikia vitendo vya utekaji nyara, unyanyasaji na madhulumu ya jinsia pamoja na mashambulizi yanayoelekezwa kwa raia.

Kutokana na watu kuhofia usalama wa maisha na mali zao, wengi wa wananchi kutoka mji wa Bayanga wamejikuta wakikimbilia msituni, kadiri ya taarifa ya Shirika la Habari za Kimissionari, FIDES. Kuna baadhi ya makazi ya watu yamechomwa moto na Makanisa kuporwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.