Jumatano majira ya jioni Papa Francisko, alimpigia simu Rais wa Italia Giorgio Napolitano,
kwa nia ya kumshukuru kwa telegram ya matashi mema aliyompekea wakati akiadhimisha
Siku Kuu ya somo wake, Mtakatifu George, siku ya Jumanne.
Na kwamba amempigia
simu, kwa sababu, Rais huyo, amekuwa ni Mfano wa kuigwa katika utendaji wa Rais
yeyote, jinsi anavyopaswa, kuiishi misingi ya umoja na ushirikiano na wengine , wakati
wa vipindi vya misukosuko na majaribu yanyotaka kuigawa jamii, na jinzi ya kuvishinda
vishawishi vya kuzua mizozo na ghasia. Na Msemaji wa Vatican, anasema
kwa mwaka huu, Papa Francisko atafanya ziara moja tu ya Kimataifa Brazil- Padre
Federico Lombardi, Msemaji wa Vatican, amebainisha kwamba, Papa Francisko atakuwa
na ziara moja tu ya kimataifa kwa mwaka 2013. Msemaji huyo ambaye pia ni Mkurugenzi
wa ofisi ya habari ya Vatican, Padre Lombardi, aliuambia mkutano wa wanahabari
uliofanyika katika makao makuu ya Ofisi ya Chama cha wanahabari cha Roma. Aliwataka
wanahabri hao wasitarajie sana matukio ya safari za Kipapa za Kimataifa kwa mwaka
huu, zaidi ya safari atakayoifanya Papa Francisko, huko Rio de Janeiro, Julai 23-28,
kwa ajii ya Maadhmisho ya SIKU YA vijana ya Dunia , itakayongozwa na Madambiu: “Nendami
na Mkawafanye watu wa mataifa yote kuw awanfunzi wangu” (Mt 28, 19). Na pia msemaji
wa Vatican , almeeleza juu ya kuchapishwa kwa waraka wa Kipapa wa kwanza wa Papa
Bergoglio, huku akikumbusha kwamba, Mstaafu Benedict XVI, alikuwa tayari ameandaa
mengi juu ya mada ya imani, tunayoiadhimisha mwaka huu. Na kwamba , Papa Mstaafu,
ambaye kwa sasa anakaa katika Castel Gandolfo, unatarajiwa kurejea katika makazi yake
, katika Monasteri ya Mama wa Kanisa , mwishoni mwa April au Mei mapema. Na Papa
Francesco, ataendelea kuishi katika jengo la Mtakatifu Marta, ambako, anajisikia
vizuri hadi itakapo tangazwa vinginevyo. Na pia hivi karibuni mismamizi wa safari
za Kipapa Dr. Alberto Gasbarri, ambaye ni msimamizi mkuu katika safari za Papa, yuko
katika maandalizi ya safari ya kwenda Rio de Janeiro, kwa ajili ya matayarisho ya
ziara ya Papa Francisko. Baba Mtakatifu Francisko atashiriki katika sherehe na Ibada
ya Mkesha wa Vijana na njia ya Msalaba kwa ajili ya kufunga adhimisho la Siku ya Vijana
ya Dunia kama ilivyopangwa tarehe kufanyika jumapili Julai 28 , katika uwanja wa Imani
wa Guaratiba, Brazil.