2013-04-25 13:46:10

Msijifungie katika ubinafsi, kuweni wazi na sikilizeni wengine!


Katika kipindi hiki cha athari za myumbo wa uchumi kimataifa, watu wengi wanaonekana kukata tamaa kiasi hata cha kukosa dira katika maisha. Kimekuwa ni kipindi cha taabu na mahangaiko kwa familia nyingi hasa kutokana na ukosefu wa fursa za ajira, hali ambayo inakwamisha mipango ya watu wengi, hali ambayo pia imepelekea kumong'onyoka kwa misingi ya maadili na utu wema. Baadhi ya watu wanatafuta njia za mkato katika maisha!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, twitter anasema kwamba, katika kipindi hiki cha athari za myumbo wa uchumi kimataifa, hakuna haja mtu kujifungia katika ubinafsi, bali kujiweka wazi na kuwasikiliza wengine.







All the contents on this site are copyrighted ©.