2013-04-25 09:46:54

Kanisa ni Jumuiya ya Upendo na si urasimu wa shirika


Kanisa si urasimu wa shirika , lakini ni historia ya upendo, Papa Francisko, alieleza wakati wa wakati wa Ibada ya Misa, mapema Jumatano katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta cha Mjini Vatican, katika mfululizo wa Ibada anazoziongoza mapema asubuhi kwa ajili ya Wafanyakazi wa Vatican. Ibada hii ilihudhuriwa na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha Kujitegemea kinachosimamia masuala ya fedha na uchumi wa Vatican( IOR). Papa Francisko, aliadhimisha Ibada hii akisaidiwa na Kardinali Javier Lozano Barragán, Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma kichungaji kwa wafanyakazi katika Idara za Afya.

Homilia ya Papa, ilitazamisha katika masomo ya Siku , yaliyozungumzia jumuiya ya kwanza ya Wakristu, ambayo iliendelea kukua na wafuasi kuongezeka. Papa akisema lilikuwa ni jambo jema, lakini pi alionyesha kusikistika kwamba walifanya “mikataba" ili kupata hata washirika zaidi katika wa jumuiya hizo.

Papa aliasa na kutoa maelezo kwaba, hiyo haikuwa njia kanisa linamopaswa kutembea, kwani njia aliyopenda Yesu, kanisa lake kutembea ndani yake ni njia nyingine, ni njia ngumu, njia ya msalaba na mateso, ambayo wakati mwingine hutufanya sisi kujiuliza, kanisa ni nini ? Amesema, Kanisa hili ni sisi , lakini haliundwi na sababu za matakwa ya binadamu, ila huundwa na Kristu mwenyewe,

Papa alisisitiza, Kanisa, si wafuasi wanaolifanya kanisa , lakini wao ni wafuasi wa Yesu Kristo, ni mitume wa Yesu ambaye nae ni Mtume wa Baba wa Mbinguni.

Kwa hiyo, unaweza kuona kwamba, Kanisa huanzia hapo, katika moyo wa Baba, aliye asili ya wazo hili, Baba mwenye upendo. Ndiye mwanzo wa historia hii ya upendo wa nyakati zote na bado unaendeleo bila ukomo. Kwetu sote wake kwa waume ni sehemu ya upendo huu , kila mmoja akiwa ni kiungo katika mnyonyoro huu wa upendo , Na kama hatuwezi kuelewa hili, basi hatuwezi kuelewa kanisa ni kitu gani.

Papa aliendelea kusema, katika majaribu Kanisa huwezeshwa kukua bila kupoteza njia ya upendo, kwa kuwa, kanisa halikui kwa nguvu za binadamu. Papa aligusia udhaifu wa Binadamu katika akisema, "lakini baadhi ya Wakristu, katika majaribu haya, hukosea na kuchukua njia zisizo sahihi, kama historia inavyoonyesha , waligeukia njia za kibinadamu , mfano kuuunda jeshi la Kanisa na kufanya vita vya kidini , kinyume na Kanisa la Mungu, ambalo ni upendo . Kwa makosa hayo, sisi pia twapaswa kujifunza makosa yetu, katika historia hii ya upendo.
Basi kama ndivyo pengine tunajihoji kwa njisi gani basi Kanisa litakua? hakuna sabubu za kuhofia kwani Yesu Kristu mwenyewe alitoa jibu tena kwa lugha nyepesi kwamba, Kanisa litakua kama mbegu ya haradali, au kama ilivyo chachu ndani ya unga, huumuka bila kelele. Kanisa hukua polepole tokea chini.

Mwisho wa Homilia yake aliwageukia wafanyakazi katika Idara ya fedha na Uchumi ya Vatican( IOR), akisema , wakati Kanisa likujivunia mpanuko wake na kulazimika kutengeneza mifumo ya utendaji , kama shirika, hili la IOR na ofisi zake kuwa na urasimu,ulazima huo ,haupaswi kulifanya Kanisa kupoteza msingi wake mkuu wa kuwa chombo cha upendo. vinginevyo kuna hatari ya Kanisa kugeuzwa kuwa shirika au chama cha kujitegemea( NGO).

Papa amesisitiza, kamwe Kanisa sio NGO. Kanisa ni historia ya Upendo, licha ya kuwa na kitu kama IOR, ambacho kweli ni muhimu na, ofisi zake zinahitajika, kama kituo rejea katika utoaji wa msaada kwenye historia hii ya upendo. Lakini Papa aliasa, utendaji wote wa Mashirika na ofisi za Kanisa unapaswa kuzingatia upendo wa kanisa ,na si kutenda nje ya hilo kama NGO, kwani utendaji kama NGO, si njia sahihi ya Kanisa.

Papa aliendelea kufafanua juu ya hilo akitolea pia mfano wa Mama nyumbani kwamba yeye si mratibu wa nyumba yake, lakini ni Mama. Na Kanisa ni mama. Na sisi tumo katika historia hii ya upendo inayo songa mbele kwa nguvu za Roho Mtakatifu , na sisi wote pamoja ni familia moja katika Kanisa ambaye ni mama yetu. "
Na mwisho kabisa, aliinua sala kwa Mama Bikira Maria, akiomba neema ya furaha, furaha ya kiroho ya kudumu katika njia hii ya historia hii ya upendo."








All the contents on this site are copyrighted ©.